Baadhi ya Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wameelezea tuhuma zilizozagaa mtaani kuwa baadhi ya wabunge wanarekodi mambo yanayoendelea bungeni na kuzisambaza katika mitandao ya kijamii kwa kutumia simu za mkononi.
Baadhi ya wabunge hao wamesema kuwa wanalazimika kurekodi bunge kwa kutumia simu zao kwa kile wanachokidai kuwa ni kuweza kupata taarifa zinazoendelea bungeni waweze kuwatumia wananchi wao ili waweze kujua wawakilishi wao wanatoa hoja gani bungeni.
Wabunge wengine wamelalamikia kitendo hicho ni kinyume cha utaratibu kwani vitu vingine vinavyorekodiwa havipendezi kwenda moja kwa moja kwa wananchi wakidai kuwa habari huandaliwa na watu wenye taaluma na waliopata ujuzi wa Uandishi wa Habari lakini si kila mbunge anaweza kuwa na taaluma ya kuandaa habari.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni