Ijumaa ya May 6 2016 kama ni mtumiaji wa mitandao ya kijamii hususani Whatsapp najua utakuwa ulipokea ujumbe ambao ulikuwa unaripotiwa kuwa umetoka kwa meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita, ujumbe uliokuwa umeenea ulikuwa unahusisha kuwa meya wa Dar es Salaam Isaya Mwita ametangaza sheria mpya.
Meya Isaya Mwita ameongea na millardayo.com
na kueleza kuwa ujumbe unaoenea kuwa ametangaza sheria mpya Dar es
Salaam sio wa kweli na umetungwa na watu ambao wanapanga kumchafulia
jina lake.
Ujumbe wa uongo ambao ulisambazwa leo May 6 2016 na kudaiwa umetoka kwa meya wa Dar es Salaam
“Sio
kweli kuwa kuna sehemu nimetoa statement ya namna hiyo ila huyo
atakayekuwa ameandika atakuwa na lengo tofauti, kwa hiyo naomba wananchi
wapuuze hiyo statement ambayo imekuwa ikisambaa, bahati mbaya sikuwahi
kupata mtu akiuliza maoni yoyote kuhusiana na tukio hilo la Kimara ila
kwa upande wangu sijatoa tamko lolote”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni