Jumanne, 10 Mei 2016

mabasi ya mwendo kasi yaanza

ImageMabasi ya mwendo wa kasi TZ

Huduma ya mabasi ya uchukuzi yanayoenda kwa kasi BRT nchini Tanzania imeanza rasmi siku ya jumanne katika jiji la kibiashara la Dar es Salaam.

Abiria watalipa shilingi 400 na 800 huku wanafunzi wakilipa 200 kulingana na mamlaka ya uchukuzi wa barabarani na majini SUMATRA.

ImageKituo cha mabasi ya mwendo wa kasi Tanzania

Mkurugenzi mkuu anayesimamia mamlaka hiyo bw Giliard Ngewe amewaambia maripota mjini humo kwamba nauli zitakuwa shilingi 400 kwa uchukuzi wa barabara ndogo,650 kwa barabara kuu na shilingi 800 kwa uchukuzi wa barabara kuu na ndogo huku wanafunzi wakilipa shilingi 200 kwa kila safari.

ImageAbiria wakiwa wamepanda basi la BRT

ASiku ya Jummanne na Jumatano mabasi hayo yatahudumu kati ya saa kumi na moja alfajiri na saa sita mchana.

ImageKituo cha mabasi ya BRT Tanzania

Tunawaonya wanaoendesha pikipiki na madereva wa magari mengine kutotumia barabara za mradi wa BRT,alisema akiongezea kwamba bado wanazungumza na washikadau kutafuta njia nzuri ya kupanga barabara zitakazotumiwa na BRT na mabasi mengine ya abiria.

Kulingana na yeye,mfumo huo wa BRT hauyaruhusu mabasi mengine kutoa huduma pamoja na mabasi ya BRT kwa hivyo abiria walioko katika barabara za BRT hawataruhusiwa kutumia mabasi mengine.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Ads Inside Post