Jay Z alitoka na binti yake Blue Ivy ambae alivalishwa kama Billie Jean wa Michael Jackson.
Nyota wengi wa sanaa ya filamu na muziki nchini Marekani wakiwa na familia zao wamesherehekea siku ya Halloween kwa kuvaa mavazi ya ajabu, kutisha, kuvutia na mengine yenye kupendeza.
Jay Z na mkewe Beyonce walimvalisha mtoto wao Blue Ivy kama Billie Jean, moja ya nyimbo aliyowahi kuimba gwiji wa Pop Michael Jackson, mtoto wa Kanye, North West naye alivalishwa nguo za ajabu na zenye kuvutia huku mama yake Kim Kardshian akiwa amevaa nguo yenye picha fuvu la binadamu.
Hivi ndivyo baadhi ya mastaa walivyosherehekea siku hiyo inayoadhimishwa Oktoba 31 kila mwaka.
Beyonce akimbusu mwanae kipenzi Blue Ivy aliyevalishwa kama Billie Jean.
Billie Jean mwenyewe Michael Jackson wakati wa uhai wake.
North West ambaye ni mtoto wa Kanye West akiwa amevalishwa mtindo wa kipekee katika sikukuu hiyo.
Mariah Carey akiwa na wanae mapacha.
Mkali wa “I was born to make you happy” akifurahia na watoto wake pamoja na mama yake.
Kim Kardashian akiwa na mwanae pamoja na rafiki yake.
Malkia wa Mitandao ya Kijamii Kim Kardashian naye hakuwa nyuma.
Mel B wa kundi la zamani la Spice Girls akiwa na mumewe Stephen Belafonte pamoja na familia yao ndani ya Halloween.
Adele akiwa mumewe kwenye sikukuu hiyo ya Halloween.
Kylie Minogue naye alitokelezea kiivyo.
Taylor Swift naye alibabaisha kwa kivazi chake chenye mabaya.
Katy Perry, mwanamuziki kutoka Uingereza naye aliamua kushangaza watu kwa kivazi chake cha ajabu.
Mtalaka wa Wiz Khalifa Amber Rose, vituko vitupu.
Binti anayetoka familia y kitajiri inayomiliki hoteli za Hilton duniani, Paris Hilton naye alibamba sawa sawa.
Muigizaji Jessica Alba naye aliamua kusherehekea kwa kuvaa wigi kubwa huku akiambatana na rafiki yake Kate Hudson.
Mwanamuziki wa Pop mwenye vituko Lady Gaga aliamua kusherehekea kawaida siku hiyo tofauti na alivyozoeleka.
Halloween ni sherehe ya kila mwaka ambayo hufanyika katika mataifa kadhaa kila Oktoba 31, ambayo ni siku kabla ya kufunga kwa Wakristo wa Magharibi kwa siku zote za Hallow.
Ni wakati ambao watu hukumbuka wafu, wakiwemo watakatifu (hallows), watu waliouawa bila hatia, na watu wenye imani waliotangulia.
Watu wanaosherehekea siku hiyo hufanya mizaha na ujinga ili kupambana na nguvu ya kifo.
Neno Halloween lilianza tangu mwaka 1745 na lina asili ya Ukristo. Maana yake ni “Jioni Tukufu” (Holy Even)

Neno Halloween lilianza tangu mwaka 1745 na lina asili ya Ukristo. Maana yake ni “Jioni Tukufu” (Holy Evening).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni