Mgodi wa Dhahabu wa Geita Gold (GGM) kwa
kushirikiana na Tume ya kupambana na Ukimwi nchini (TACAIDS) imemteua
Staa wa kugani mashairi bongo Mrisho Mpoto kuwa balozi wa kampeni ya Kili Challenge.
Kili Challenge ni Kampeni inayolenga
kukusanya fedha kwa ajili ya kutunisha mfuko wa mapambano dhidi ya VVU
na UKIMWI. Mpoto ameteuliwa kuwakilisha na kuitangaza kampeni hii ili
kusaidiana na serikali pamoja na wadau mbalimbali ndani na nje ya
Tanzania.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni