Jumamosi, 7 Mei 2016

mchezaji wa mpira wa cameroom afia uwanjani

ImagePatrick Ekeng kushoto

Mchezaji wa soka ya kimataifa kutoka Cameroon, Patrick Ekeng, amefariki baada ya kuanguka uwanjani katika ligi ya Romania.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 alipoteza fahamu dakika saba tu baada ya kuingia uwanjani kuchukua nafasi ya mchezaji mwingine katika timu yake ya Dinamo Bucharest katika mji mkuu wa taifa hilo, Bucharest.

Hakuwa amegusana wala kukaribiana na mchezaji mwingine alipoanguka uwanjani.

ImageRafikiye Ekeng Mbia akitoa salamu zake za rambirambi katika mtandao wa Twitter

Matabibu walimkimbiza hospitalini ambako madaktari walijaribu kumfufua kwa zaidi ya saa moja bila kufaulu.

Kwa muda wa miaka michache iliyopita wachazaji kadhaa Waafrika wamefariki walipokuwa wakicheza uwanjani.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Ads Inside Post