ImageAFPImageCord inawataka viongozi wa tume ya uchaguzi wajiuzulu
Polisi jijini Nairobi wametumia mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji wa muungano wa upinzani Cord waliokuwa wameandamana hadi afisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (IEBC).
Waandamanaji hao, wakiongozwa na viongozi wa muungano huo, walitaka kuwashinikiza wakuu wa tume hiyo wajiuzulu.
Kiongozi wa Cord Raila Odinga, aliyekuwa wakati mmoja waziri mkuu, amesema viongozi hao hawawezi kusimamia uchaguzi huru na wa haki mwaka ujao.
Hii ni mara ya pili kwa muungano huo kufanya maandamano hadi afizi za IEBC.
ImageAFPImageMuungano wa Cord unapanga kufanya maandamano kila wiki
Mwishoni mwa mwezi uliopita, polisi waliwatawanya tena kwa kutumia vitoa machozi.
Viongozi wa muungano huo wameapa kufika katika afisi za IEBC Jumatatu kila wiki hadi viongozi wa tume hiyo waondoke afisini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni