Ijumaa, 3 Machi 2017

Kushamiri kwa makundi ya biashara za ngono kupitia mitandaoni, serikali iko wapi


Leo kuna jambo napenda tulijadili kama jamii kupitia hapa kwenye jukwaa letu lenye hadhi kitaifa na kimataifa.

Niende kwenye mada, nimekua mtumiaji wa mitandao ya kijamii kwa siku nyingi kidogo, natumia Whatsapp, natumia Instagram,Facebook na Jamiiforums n.k

Katika mitandao hii kuna biashara ya ngono imeshamiri siku za hivi karibuni, sisemi kwamba hiyo biashara haikuwepo, ilikuepo ila kwa sasa inakua kwa kasi ya ajabu na bila kificho kama mwanzo.

Ntakupeni mifano, kama wewe ni mtumiaji wa Facebook kwa sasa kuna pages kibao zinazojishughulisha na biashara hii haramu inayokwenda kinyume na maadili ya kitanzania.

Mojawapo ya page maarufu ambayo nimekua nikiiona ni hii "Chura hainaga ushemeji" na kuna pages zingine nyingi tu ambazo unaweza kujikuta kuna mtu ame-share inatokea kwenye wall yako.
Katika hizo pages kuna kua na picha za utupu japo sio kwa 100% ila ni picha zinazoashiria kuibu hisia za ngono kwa wanaume, pia katika hizi page kuna namba za mawasiliano za mitandao mbali mbali kama Tigo, Voda, Air tel n.k

Namba hizi zinaambatana na ujumbe flani, kwa mfano anaandika 
"Nina hamu na Mme wa mtu, kama umenipenda nitafute kwenye namba 0655XXXXXX.
Screenshot_20170303-005646.png 

Ukiachana na pages kumezuka tabia za wanawake kufata wanaume inbox na kuwatumia picha za utupu, then mwisho wa siku ni kuomba ahadi ya kuonana ili kufanya ngono, hata hivyo ahadi hizi zinaambatana na kuomba pesa.

Pia kuna wadada wengine anakufata inbox anakuuliza umeoa? Na maswali mengine ya kipuuzi kweli kweli.

Mwingine anakutumia picha zake kisha anakuomba vocha, mara najisikia kuumwa naomba pesa nikatibiwe the nikipata nafuu nakuja kwako.

Hebu watanzania wenzangu tujiulize hii hali imetokana na nini?
Tumesikia na kushuhudia biashara ya kuuza miili ikipigwa vita katika majiji yetu kama DSM, Mwanza n.k 

Pia tumeshuhudia wanaume wanajitangaza kama mashoga wakitafutwa na serikali kuanzia huko Instagram ( refer James delicious), kwanini serikali hii hii isishughulike na hizi biashara za hawa wadada? Maana kwa sasa namba za simu zimesajiliwa tofauti na zamani.
Kwanini serikali kupitia vyombo vyake isianzishe vitengo vya kupambana na biashara ya ngono kwa njia ya mtandao? Maana sasa madada poa na makaka poa wameanza kua wabunifu zaidi, badala ya kukaa buguruni kusubiri wateja, saivi wanafungua pages zao na kuweka namba ili watafutwe na wateja wao. 

Serikali isikae kimya, jamii tusikae kimya hili suala linakua siku baada ya siku, maadili yetu yanaporomoka kwa kasi.

Tumeona serikali ikifuatilia na kuwapata watu wanatoa lugha chafu mitandaoni hasa Facebook, kwanini haifatilii hili mbona nalo linakiuka sheria na maadili yetu? 

Watoto wetu, wadogo zetu, ndugu zetu wengi wako katika mitandao hii, mzazi amka usijekukuta binti yako anayesoma Form 3 ndiye group admin wa page ya Chura hainaga ushemeji.

Tufatilie kwa makini watoto wetu, haiwezekani mtoto wa kike ananitongoza inbox Facebook? Hili ni tatizo watanzania jamii inakua ya kihuni hii, mtoto wa sekondari anapata wapi ujasiri wa kutongoza mwanaume? 
Mzazi usiogope kuonekana mkoloni, mpangie mwanao ukomo wa matumizi ya simu yake, akitaka Uhuru 100% asubiri akiwa na mji wake

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Ads Inside Post