



RAPA maarufu wa ngoma ya Get At Me Dog, Dark Man X ‘DMX’ mwenye umri wa miaka 45 amepata mtoto wa 15 na wa kiume Ijumaa iliyopita (Agosti0 19) kupitia kwa mpenzi wake wa siku nyingi, Desiree Lindstrom.
Kwa mujibu wa taarifa zilizochapishwa na jarida la TMZ, mtoto huyo ambaye ni wa kwanza kwa mwanadada Desiree na wa 15 kwa DMX alizaliwa akiwa na uzito wa Kilogram 2.9 na amempa jina la Exodus Simmons.

Mwaka 2010, DMX alikorofishana na aliyekuwa mkewe Tashera Simmons hivyo kulazimika kuachana akiwa ameishi naye kwa muda wa miaka 11.

Mwaka 2013, alitangaza mahakamani kuwa amefirisikajambo ambalo lilitafsriwa kuwa ni moja ya njama zake za kukwepa kuwahudumia watoto wake. Mwaka 2015, alihukumiwa kwenda jela miezi 6 kwa kushindwa kulipa pesa kiasi cha dola $400,000 kwa ajili ya matunzo ya mwanaye.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni