Jumatano, 1 Machi 2017

AliKiba Amaliza Kurekodi Kolabo Yake na Yvonne Chaka Chaka


Msanii wa Bongo Fleva Ali kiba amemaliza kurekodi Kolabo yake na Msanii nguli wa muziki barani Afrika Yvonne Chakachaka leo huko nchini Afrika Kusini.

Ali Kiba ambae yupo Afrika Kusini kwenye ziara yake ya kimuziki kwenye miji tofauti tofauti amekamilisha project hiyo na Mwanamama Yvonne ya kufanya kazi pamoja ambayo Kiba alieelezea tangia mwaka jana.

Akithibitisha kukamilika kwa Kolabo hiyo Ali Kiba kupitia Ukurasa wake wa Twitter ameandika “We done with Mama @yvonne_chakachaka . I am honored and truly excited about our project . Thank you Mama for everything #KingKiba

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Ads Inside Post