Jumatano, 1 Machi 2017

Rais Magufuli amteua Bi. Salma Kikwete kuwa Mbunge

TAARIFA KIVA VYOMBO VYA HABARI

Ikulu, Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 01 Machi, 2017 amemteua Mhe. Salma Kikwete kuwa Mbunge wa Viti Maalum wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mhe. Salma Kikwete ni Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.

Mhe. Salma Kikwete ataapishwa kwa mujibu wa sheria na taratibu zitakazotangazwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais,IKULU
01 Machi, 2017

Dar es Salaam
[​IMG]

Masahihisho ya Ikulu:

Mama Salma Kikwete ameteuliwa kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na SIO Mbunge wa Viti Maalum

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Ads Inside Post