Msanii Ali Kiba amefika nchini leo akitokea Afrika Kusini. Baada ya kufika uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere alipokelewa na mashabiki wake.
Katika hali ya kushangaza msanii huyo amepanda juu ya gari na kushikilia tuzo yake kujigamba kwa mashabiki wake.
Kitendo hiki kinahatarisha maisha yake na maisha ya wengine wanaotumia barabara. Hatari hiyo ni zaidi ya kutofunga mkanda, kuendesha gari lisilo na breki, tairi lenye kipara etc.
Sheria za usalama barabarani haziruhusu ujinga huu hivyo msanii huyu achukuliwe hatua kali sana.
Kitendo alichokifanya ni zaidi ya dereva wa Itigi au Diamond Platnumz.
Jela inamnukia.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni