Mtaalamu mmoja wa kompiuta raia wa Nigeria anasema kuwa alilazimika kufanya mtihani kwenye uwanja wa ndege wa JFK mjini New York, ili kuwaridhisha maafisa kuwa kweli alikuwa na utaalamu huo.
Kulingana na mtandao wa LinkedIn, Celestine Omin mwenye umri wa miaka 38, aliwasili uwanja wa JKF mjini New York siku ya Jumapili, baada ya safari ya saa 24 kutoka nchini Nigeria.
Kampuni hiyo huwaajiri watu wenye vipawa vya ufundi wa kampiuta barani Afrika, na kuwaunganisha na waajiri nchini Marekani.
- Amri ya Trump: Ni nani anaathirika?
- Ndege zatakiwa kubeba abiria wa nchi 7 za Waislamu kueleka Marekani
Mkurugenzi wa Facebook Mark Zuckerberg alitembelea ofisi za Andela wakati alifanya ziara nchini Nigeria mwaka uliopita.
Bwana Omin anaripotiwa kupewa visa ya muda mfupi kufanya kazi katika kampuni ya First Acces iliyo eneo la Manhattan mjini New York.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni