1)KUJIBU UJUMBE WA SIMU
Kama mwanaume atajibu ujumbe wa simu katikati ya tendo au wakati akimuandaa mwenzi wake kabla ya tendo au dakika chache baada ya kumaliza tendo, mwanamke anaweza kuchukulia kitendo hicho kama vile hathaminiwi na mwanaume huyo na atachukulia kitendo hicho kama vile mwanaume huyo anamtumia tu kumaliza matamanio yake ya ngono ingawa hatasema. Lakini kama kitendo hicho kikifanywa na mwanamke, mwanaume atakichukulia kama vile amedharauliwa kupita kiasi na kinaweza kimsababishi mwanaume kukosa msisismko wa kuendelea na tendo au hata kama akiendelea hatokuwa na ufanisi kama alivyokusudia.
2)KUTAJA JINA LA MWINGINE
Kuna wakati mwanamke anaweza kumwambia mpenzi wake wawapo kitandani, kwamba mpenzi wa rafiki yake huwa anamfanyia huyo rafiki yake hivi au vile wanapokuwa kitandani na angependa na yeye afanyiwe hivyo na huyo mpenzi wake. au anaweza kumwambia mpenzi wake vile alivyokuwa akifanyiwa na mpenzi wake wa zamani waliyeachana na akataka afanyiwe hivyo. Hilo ni kosa kubwa sana kutaja wanaume wengine ukiwa na mwenzi wako au mpenzi wako kitandani na wala usije akavuta taswira ya mwanaume mwingine unayempenda wakati wa kufanya tendo ili ufike kileleni, kwani unaweza kujikuta ukitaja jina la huyo mwanaume na kuzua balaa. Mazungumzo yako na mashoga zako kuhusu ngono yaweke pembeni kwanza wakati unapojamiiana na mwenzi wako.
#3)KUMWAMBIA MPENZI KWAMBA ULIJIFUNZA MAHALI FULANI
Sio vibaya kama utajifunza mambo fulani fulani kuhusu mbinu za kujamiiana kwa ufanisi kupitia magazeti au majarida, lakini si vyema kumwambia mpenzi wako kwamba mbinu fulani na fulani kuhusu kujamiiana ulijifunza kupitia gazeti au jarida fulani. Kufanya hivyo kutamfanya mpenzi wako akuone kama vile wewe sio mbunifu na mtundu kitandani mpaka ukatafute kwenye magazeti.
4) KUOMBA RADHI KABLA YA TENDO KWAMBA ULISAHAU KUNYOA
Kumuomba radhi mwanaume kwamba ulisahau kunyoa nywele za sehemu zako za siri wakati mkijiandaa kufanya tendo kunaweza kumkwaza mwanaume kwa sababu wapo wanaume ambao hupenda sana kujamiaana na wanawake ambao nywele za sehemu zao za siri hazijanyolewa kipara kabisa, kwa maana ndio kwanza zinachipua au zimekua kidogo lakini sio msitu. Sasa unapomuomba radhi kwamba ulisahau kuvyoa, je unajuaje kama hapendi hizo nywele za chini? Kumbuka kwamba sio kila kinachokukera kuhusu mwili wako kitamkera na mwenzako.
5)UKIMYA KUPITA KIASI
Wanawake wengi wanajisikia aibu kupiga makelele wakati wa tendo. Usifanye hivyo. Wanaume hupenda sana wanawake wanapopiga makelele wakati wa tendo. Naomba nieleweke, sio makelele ya kuigiza, nazungumzia yale makelele yanayokuja yenyewe bila kulazimisha kwani pale inapokuja hali ya kutaka kupiga kelele kutokana na kunogewa na tendo kisha ukajitahidi kuzuia, ukweli ni kwamba hutalifurahia tendo na badala utaelekeza akili yako katika kuzuia kufanya kile ambacho hisia zina kulazimisha kukifanya.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni