Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo siasa. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo siasa. Onyesha machapisho yote

Jumatano, 1 Machi 2017

TRA yamwita Mbowe mahakamani kisa hakutumia EFD ktk Club ya Bilcanas

 20170302_042800.jpg

Bila shaka naona hizi siasa hadi kwenye vyombo vya serikali na hili halijaanza Leo:

Nakumbuka kanda ya ziwa mmiliki wa Imalaseko yalishamkuta baada ya kushabikia upinzani TRA walivamia na kumfilisi.

Na wengine wengi ukiwa upinzani ukiisema vibaya chama tawala na serikali basi jamaa wanatumwa.

Kwa hali ya kawaida na kulingana na sheria za nchi Bilcanas inamilikiwa na Mbowe hotels ni kampuni kwanini wasiishitaki kampuni badala ya mtu?

Kampuni ni legal person na inataratibu zake kwanini afuatwe mmiliki badala ya kampuni?

Mbona kwa Dangote walifuata taratibu za kuwawajibisha na hawakumshitaki Dangote kama mmiliki wa campun

mbunge atoa pendekezo condom zipigwe marufuku tanzania

[​IMG]
Mwakilishi Nadir Abdul-latif Yussuf Alwardy, CCM wa Jimbo la Chaani aliitaka Serikali ya Zanzibar kupiga marufuku Condoms, uuzwaji na usambazaji ikiwa kweli jamii inataka kulidhibiti tatizo la ubakaji na udhalilishaji wa jinsia kwa vijana na watoto.
Amesea kuzagaa kwa Condom mitaani ni kichocheo kikubwa kinachowamasisha vijana kufanya vitendo vya kudhalilishana ovyo ovyo wakijua kuwa wao watabaki salama.

Alisistiza kuwa matumizi ya Condom yatumike kwa kibali maalum cha Daktari tu.

yanga na simba zilivyogonganisha viongozi wa siasa na serikali












Hivi ndivyo timu za yanga na simba zilivyowakutanisha baadhi ya viongozi wa serikali pamoja na viongozi wa chama cha upizani cha chadema









Jumatano, 11 Mei 2016

waziri mkuu atimuliwa bungeni

ImageGETTYImageWaziri mkuu wa New Zealand

Waziri Mkuu mpya wa New Zealand John Key ametupwa nje ya bunge na spika baada ya kukaidi kufuata kanuni za bunge.

Bunge hilo limekua na mjadala mkali kuhusu sakata ya akaunti za siri ambazo zinadaiwa kuwepo kisiwa cha Panama.

Spika wa Bunge David Carter ametetea hatua yake na kusema Waziri Mkuu alikaidi onyo la kutoheshimu kanuni za bunge, na hivyo hakua na kinga ila kumuadhibu, kama wabunge wengine.

Rekodi za bunge zimenakili kwamba Waziri Mkuu huyo aliwahi kutupwa nje ya bunge mara tatu wakati akiwa mbunge.

Hata hivyo si mara ya kwanza Waziri MKuu NewZealand anatupwa nje ya bunge.

Waziri Mkuu wa zamani Helen Clark alitupwa nje mwaka 2005 huku naye mtangulizi wake, David Lange akijipata pabaya miaka ya 1986 na 1987.

Jumatatu, 9 Mei 2016

waislamu wamjia juu Trump

ImageDonald Trump

Baraza la uhusiano mwema la kiislamu nchini Marekani limemtaka mgombea wa urais kwa tiketi ya chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump, kuomba msamaha kwa kuamrisha mwanamke wa dini ya kislamu kufurushwa kutoka kwa mkutano wake wa kisiasa.

Rose Hamid alilalamikia wito wa bwana Trump wa kuweka marufuku ya muda kwa waislamu wanoingia nchini Marekani.

Wafuasi wa Trump walipoketi, mwanamke huyo alisimama kwa ukimya, huku akivalia vazi lililokuwa na maandishi, salaam. Nimekuja kwa amani.

ImageWafuasi wa Trump wakimzoma mwanamke wa Muislamu aliyefurushwa katika mkutano wake.

Umati uliyokuwemo ulifanya kelele za kejeli na maafisa wa usalama wakamwondoa.

Bi Hamid mwenye umri wa miaka 56 na ambaye anafanya kazi ya huduma katika kampuni ya moja ya ndege ,baadaye aliamrishwa na afisa mmoja wa usalama kuondoka.

Alizomwa wakati alipokuwa akifurushwa katika mkutano huo.

mbunge apewa maji machafu na wapiga kura wake na yeye anywe

Wakazi wa Kijiji cha Nala na vitongoji vyake juzi walimpelekea maji machafu Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Anthony Mavunde wakimtaka ayanywe kwa kuwa ndiyo wanayotumia.

Mavunde alikutana na mkasa huo muda mfupi alipoingia kwenye kijiji hicho umbali wa kilomita tisa nyakati za jioni, ambako wakazi wa eneo hilo walikuwa wakimsubiri tangu asubuhi.

Mama mmoja aliyekuwa eneo hilo, alifika na chupa ya maji akimtaka Naibu Waziri ayaonje mbele yao, kwani nao ni binadamu kama yeye na wanayatumia, lakini Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Dodoma Mjini, Paul Luhamo alimzuia kuyanywa.

Pamoja na taarifa ya kijiji iliyotolewa na Ofisa Mtendaji wa Kata, Mathias Ndologa, wakazi hao walilipuka na kupiga kelele wakiipinga taarifa hiyo kwamba iligusa kwa juu matatizo yao, lakini ikaacha jambo kubwa la maji.

Kwenye risala yake, Ndologa alikuwa ameelezea suala la maji, umeme, miundombinu na upungufu wa madawati, lakini kelele zilizidi kutoka kwa wananchi wakisema jambo la msingi kwao ni moja tu, yaani maji.

Muda mfupi kelele zilianza watu wakitaka kuuliza mambo waliyoyaita ni ya msingi, ndipo Mavunde akaamuru wapewe nafasi ya kuuliza kwanza kabla hajasimama kuwasalimia.

Mmoja wa wauliza maswali alikuwa Daudi Lusinde, ambaye alieleza namna wakazi wa kijiji hicho wanavyopata adha kubwa katika kutafuta maji ambayo aliyaita ni kama dhahabu kwao.

Lusinde alisema wamepata tabu hiyo kwa muda mrefu na bado hawajaona mwanga wa matumaini zaidi ya kuendelea kuumia huku ndoo ya maji ikifikia bei ya Sh500.

“Bei ya sukari inapanda kila kukicha, lakini siyo shida hapa tatizo ni maji, mheshimiwa sisi tunanunua maji kwa gharama kubwa na ukishindwa kiasi hicho unalazimika kuchangia maji na mifugo sijui kama tutapona,” alisema Lusinde na kusababisha mkutano kulipuka kwa shangwe.

Uongozi wa kijiji na chama wilaya ulizuia kelele za vijana waliomtaka mbunge huyo aende hadi maeneo wanayochota maji akajionee, ikiwamo uchafu wa maji pamoja na umbali wake.

Akijibu hoja hizo, Mavunde alieleza kusononeshwa na kuahidi kuanzia leo ataanza kutekeleza ahadi yake hiyo kabla ya kufanya jambo lolote.

“Kwa kweli maji ni moja ya ahadi nilizoahidi kwenu, kesho ni Jumapili siyo siku ya kazi, lakini kuanzia keshokutwa (Jumatatu) nitaleta hapa wataalamu kuanza kuchimba kisima kwa gharama zangu,” alisema Mavunde.

Huku akiwa amesimama na maji aliyopewa, alisema yuko tayari kuacha shughuli za Bunge akashirikiane nao kuhangaikia maji, hadi pale watakapoyapata na kuanza kujenga matangi.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mkutano huo, Naibu Waziri alisema katika kipindi cha kampeni alifika eneo hilo na kuahidi kuwapatia maji, lakini muda ulikuwa bado. Hata hivyo, Serikali ya awamu ya tano ina miezi sita madarakani.

“Hiyo ilikuwa ni sehemu ya ahadi yangu kwenye kampeni, kwa hiyo matatizo ya maji hapa nayajua na kweli ni makubwa, ndiyo maana nimeamua kuvuruga kila ratiba ili niokoe watu hawa kweli wako kwenye mateso,” alisema.

Mhandisi wa Maji Manispaa ya Dodoma, Simon Sasala alisema kijiji hicho kina wakazi 7,600 ambao wanahitaji lita 230,000 za maji kwa siku, lakini kuna kisima kinachotoa lita 89,000 na wakati mwingine hakifanyi kazi.

Sasala alisema maji hayo hayatoshelezi kwani yapo kwa asilimia 39, hali ambayo inawapa shida hasa kina mama kutokana na wengi wao kulazimika kufuata maji ya kutumia umbali mrefu.

Jumapili, 8 Mei 2016

tatizo la sukari kwisha

ImageMichuziImageMagufuli aahidi sukari ya bei ya chini

Serikali ya Tanzania imeagiza sukari ilikukabiliana na upungufu wa sukari uliopo nchini.

Rais wa Tanzania Joseph Pombe Magufuli amesema badala ya kuwapa wafanyabiashara leseni ya kuagiza sukari kutoka ng'ambo serikali yenyewe ndio itaagiza sukari hiyo moja kwa moja.

Kauli hiyo inawadia baada ya mabohari zaidi kugunduliwa kote nchini yakiwa yamejaa sukari iliyoagizwa kutoka nje na ile iliyonunuliwa kwa wingi kutoka kwenye kampuni za kusaga sukari za humohumo Tanzania.

''Kuna mmoja ambaye amepatikana Arusha amehodhi zaidi ya tani elfu tano ya sukari naye mwengine huko Kilombero amenunua sukari yote kutoka kwa kampuni za humu humu nchini na akaficha.''

''Lakini hili ni swala la sasa tu, katika siku zijazo sukari itapatikana kwa wingi hapa Tanzania.Serikali imekwisha agiza sukari lakini hatutawapa hawa waliofilisi watanzania leseni ya kuingiza tena sukari.

''Serikali imeagiza na itauza sukari hiyo kwa bei ya chini,,,, hiyo ndio lengo la serikali '' alisema rais Magufuli huku mawananchi wakimshangilia.

Image''Katika siku zijazo sukari itapatikana kwa wingi hapa Tanzania.Serikali imekwisha agiza sukari lakini hatutawapa hawa waliofilisi watanzania leseni ya kuingiza tena sukari.''

Sukari hiyo ambayo huwa ni ya bei ya chini hubadilishwa na kisha kuvikwa magunia ya makampuni ya Kitanzania yanayosaga sukari na kisha kuuzwa rejareja.

Tumbua tumbua ya rais Magufuli imesadifiana na tangazo la Halmashauri ya ushuru ya Tanzania TRA kuwa imeanza kugawa sukari iliyoingizwa nchini kinyume cha sheria na kufichwa katika mabohari kote nchini.

TRA ilichukua hatua hiyo baada ya mwekezaji wa kibinafsi mkoani Lindi kupatikana na zaidi ya mifuko elfu tano za sukari kutoka nga'mbo.

Yamkini sukari hiyo hubadilishwa kwenye mifuko yenye nembo ya kampuni za kusaga sukari za Tanzania na kisha kuuzwa kwa bei maradufu.

obama awaasa wamarekani weusi

ImageObama amewahimiza wanafunzi 2,000, weusi kuimarisha juhudi za kupambana na ubaguzi

Rais wa Marekani Barack Obama amewahimiza wanafunzi 2,000, wengi wao weusi kuimarisha juhudi za kupambana na ubaguzi wa rangi aliosema umebakia nchini humo.

Akizungumza katika Chuo Kikuu cha Howard mjini Washington, Bw Obama alisema hali ya Wamarekani wenye asili ya Kiafrika imeimarika sana tangu yeye atoke chuo kikuu mwaka 1983.

ImageAFPImageObama awaasa weusi Marekani

Lakini alisema kuchaguliwa kwake kwa rais wa kwanza mwenye asili ya Afrika nchini humo hakujasaidia kupunguza ubaguzi wa rangi.

Bwana Obama alisema vijana hao wanapaswa kujivunia kuwa watu weusi lakini lazima wahakikishe kuwa wana mipango kambambe ya kuleta mabadiliko.

korea kutumia mabomu ya nyuklia

ImageReutersImageKorea kutumia mabomu ya nyuklia kujilinda

Korea Kaskazini imesema kuwa itatumia silaha zake za nyukilia kujilinda rais Kim Jong-unamesema.

Kiongozi wa wa taifa hilo lenye usiri mkubwa Kim Jong-un aliwaelezea wajumbe wa kamati kuu ya chama tawala Workers' Party mjini Pyongyang kuwa jeshi lao litatumia silaha hizo za kitonoradi kulinda uhuru wa taifa hilo utakapotishiwa.

ImageAFPImageMara kadhaa serikali ya Korea Kaskazini imetisha kushambulia Marekani na Korea Kusini kwa mabomu ya kinyukilia.

Aidha rais Kim jong un aliwaeleza wajumbe hao kuwa Korea Kaskazini sasa itaanza kusemezana na mataifa yaliyokuwa mahasidi wao hapo awali.

Vyombo vya habari vya taifa vimemnukuu kiongozi huyo akiambia baraza Kuu la chama cha wafanyikazi kinachotawala kuwa kunapaswa kuwepo mashauriano zaidi na Korea Kusini ili kuimarisha uelewano na kuaminiana.

Inadaiwa pia kuwa alisema kuwa serikali yake itafanya kila juhudi kupunguza kuenea kwa silaha za kinyukilia duniani ingawa taifa lake lilijiondoa katika chama cha kupunguza ongezeko la zana za kinukilia duniani mwaka 2003.

ImageEPAImageKim Jong-un aliwaelezea wajumbe wa kamati kuu ya chama tawala Workers' Party mjini Pyongyang kuwa jeshi lao litatumia silaha hizo za kitonoradi tu kulinda uhuru wa taifa

Korea Kaskazini ilifanya jaribio la silaha yake ya kinukilia miaka mitatu baadaye na kuna uvumi kuwa inatarajia kufanya jaribio la tano ili kwenda sambamba na mkutano wa baraza Kuu la Cchama tawala unaondelea hivi sasa.

Mara kadhaa serikali ya Korea Kaskazini imetisha kushambulia Marekani na Korea Kusini kwa mabomu ya kinyukilia.

wabunge watumia simu kujirekodi

Baadhi ya Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wameelezea tuhuma zilizozagaa mtaani kuwa baadhi ya wabunge wanarekodi mambo yanayoendelea bungeni na kuzisambaza katika mitandao ya kijamii kwa kutumia simu za mkononi.

Baadhi ya wabunge hao wamesema kuwa wanalazimika kurekodi bunge kwa kutumia simu zao kwa kile wanachokidai kuwa ni kuweza kupata taarifa zinazoendelea bungeni waweze kuwatumia wananchi wao ili waweze kujua wawakilishi wao wanatoa hoja gani bungeni.

Wabunge wengine wamelalamikia kitendo hicho ni kinyume cha utaratibu kwani vitu vingine vinavyorekodiwa havipendezi kwenda moja kwa moja kwa wananchi wakidai kuwa habari huandaliwa na watu wenye taaluma na waliopata ujuzi wa Uandishi wa Habari lakini si kila mbunge anaweza kuwa na taaluma ya kuandaa habari.

Jumamosi, 7 Mei 2016

kesi ya mohammed morsi yaahirishwa

Mahakama ya Misri, imeahirisha kesi ya rais wa zamani, Mohamed Morsi, na watu wengine 10, kwa mashtaka ya kutoa siri za taifa kwa Qatar.

Kesi za washtakiwa sita pamoja na waandishi wa habari wane, zitapelekwa mbele ya Mufti mkuu, hatua inayoonyesha kwamba wamehukumiwa kifo.

Mufti ataamua kama hukumu hizo zitekelezwe.Bwana Morsi hayumo kati ya washtakiwa hao 6.

Amekabiliwa na kesi kadha tangu jeshi, lilipomtoa madarakani mwaka wa 2013 na amewahi kuhukumiwa kifo.

ndugu yake bush kasema hatompigia kura Trump

Aliyekuwa mgombea wa urais wa tiketi ya chama cha Republican nchini Marekani, Jeb Bush, amesema kuwa hatampigia kura Donald Trump katika Uchaguzi wa Novemba.

Bwana Bush alisema kuwa Trump hana tabia wala mienendo ya kuwa Rais wa Marekani.

Jeb ni mojawapo wa wanachama mashuhuri wa Republican kutanganza hadharani kuwa hatompigia kura Bwana Trump kwa sababu ya kampeni yake ya kiburi ambayo imegawanya chama cha Republican.

Mnamo Alhamisi Spika wa Bunge, Paul Ryan, alisema kuwa hatamuunga mkono mfanyabiashara huyo tajiri, ingawa atakutana naye juma lijalo.

Hata hivyo Bwana Trump ameungwa mkono na mgombezi wa Urais wa zamani Bob Dole aliyeshindwa katika uchaguzi na Bill Clinton wa chama cha Democratic mwaka 1996.

Ijumaa, 6 Mei 2016

Mitandao yamcheka Mgombea urais Marekani Donald Trump kwa kutoitamka vizuri Tanzania

Mgombea Urais kupitia Republican Marekani Donald Trump anazo headlines nyingine za kushindwa kutamka vizuri neno Tanzania kwenye hotuba yake kuhusu mambo ya nje ya Marekani alipokua akizungumzia ugaidi wa balozi za Marekani Tanzania na Kenya kulipuliwa.
Kibongobongo inawezekana tusingemcheka kwa jinsi alivyoitamka ila kwa wenzetu Marekani na Ulaya naona imekua ishu, vyombo vya habari vimeripoti kuhusu kushindwa huko kuitamka vizuri Tanzania kwenye hotuba yake ya kwanza ya mambo ya nje ambapo watu wamemkejeli na kumcheka

Ads Inside Post