Vita ya Dawa za Kulevya: Steve Nyerere alivyopiga kambi Bungeni Kumuokoa Wema Sepetu
1. Steve Nyerere ndiye aliyewapa Mwigullu, Nape, Msukuma na Mlinga namba za simu za Mama Wema Sepetu
2. Nape na kundi lake waliapa kupambana na Makonda bila kumshirikisha Wema kwa vile ni mropojaji , angeweza kutoa siri. Lakini siyo siri tena.
3. Nape walifikiri kufanya hivyo ni kumuokoa Wema kwa vile alikitetea Chama wakati wa uchaguzi. Wakasahau kuwa wanakidhalilisha Chama kutetea wauza Unga tofauti na ilani ya Chama inavyosema
4. Kwa upande wake Steve Nyerere alijua akimuokoa Wema, CCM wangerudi kumbembeleza Wema kupitia kwake na hivyo angepiga pesa za kutosha
5. Steve Nyerere aliwafikia pia Wabunge wa CHADEMA wakiwemo Freeman Mbowe na Zitto Kabwe ndiyo maana Bunge lilipuka
Mytake: 1. Nape , Mwigullu wanapaswa kujitathmini kama wanastahili kuendelea kuwa viongozi waandamizi wa serikali ? Nini hatma ya Nape, Mwiggulu na Msukuma ndani ya CCM?
2. Mwigullu, Nape na Msukuma ni wana CCM waliokuwa maadui namba moja wa CHADEMA, Je Chadema wamefanikiwa kuwamaliza kisiasa? Je wanaweza kuwapokea ndani ya CHADEMA endapo CCM wataamua kutokuwa na imani nao kwa kitendo chao cha kuunganna na Wabunge wengine wa CHADEMA kutetea watuhumiwa wa madawa ya kulevya na hivyo kudhoofisha juhudi za serikali ambayo wao ni sehemu ya serikali katika kupambana na bishara ya dawa za kulevya?
3. Kwa ujumbe wa huu wa sauti kati ya Mama Wema Sepetu na Steve Nyerere na kwa kuzingatia nafaai za Nape na Mwigullu, hawapaswi kujiuzulu ili kulinda heshima ya serikali?
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni