Jumatano, 1 Machi 2017

TRA yamwita Mbowe mahakamani kisa hakutumia EFD ktk Club ya Bilcanas

 20170302_042800.jpg

Bila shaka naona hizi siasa hadi kwenye vyombo vya serikali na hili halijaanza Leo:

Nakumbuka kanda ya ziwa mmiliki wa Imalaseko yalishamkuta baada ya kushabikia upinzani TRA walivamia na kumfilisi.

Na wengine wengi ukiwa upinzani ukiisema vibaya chama tawala na serikali basi jamaa wanatumwa.

Kwa hali ya kawaida na kulingana na sheria za nchi Bilcanas inamilikiwa na Mbowe hotels ni kampuni kwanini wasiishitaki kampuni badala ya mtu?

Kampuni ni legal person na inataratibu zake kwanini afuatwe mmiliki badala ya kampuni?

Mbona kwa Dangote walifuata taratibu za kuwawajibisha na hawakumshitaki Dangote kama mmiliki wa campun

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Ads Inside Post