Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo michezo. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo michezo. Onyesha machapisho yote

Jumapili, 5 Machi 2017

kwa mara ya kwanza Calderon baada ya kuumia kichwa

Usiku wa March 3 2017 mshambuliaji wa zamani wa Liverpool na Chelsea ambaye kwa sasa anaichezea Atletico Madrid ya kwao Hispania Fernando Torres, jina lake lilitawala mitandaoni baada ya kugongwa na kupoteza fahamu uwanjani wakati wa mchezo dhidi ya Deportivo La Coruna.
Good news ikufikie kuwa Fernando Torres anaendelea poa na aliruhusiwa kutoka hospitali asubuhi ya March 3, lakini leo Torres ameonekana akihudhuria katika uwanja wao wa nyumbani wa Vicente Calderon kuangalia timu yake ikicheza dhidi ya Valencia.
Kuonekana kwa Torres uwanjani mbele ya mashabiki akiwa jukwaani kulileta furaha kwa mashabiki wa soka na kujua kuwa anaendelea vizuri na jeraha lake la kichwa, Torres aliishuhudia timu yake ikiifunga Valencia goli 3-0.
Torres alivyokimbizwa hospitali baada ya kupoteza fahamu uwanjani kutokana na kugongwa sehemu ya kichwani.

Jumatano, 1 Machi 2017

Yanga yamaliza hasira kwa Ruvu Shooting

Yanga-TanzaniaHaki miliki ya pichaGOOGLE
Image captionFuraha ya bao , Simon Msuva
Baada ya kuchapwa na watani wao wa jadi Jumamosi iliyopita, mabingwa watetezi wa taji la ligi kuu Tanzania bara Yanga Sports Club, wameibukia kwa Ruvu Shooting na kuitandika magoli 2-0 kwenye mechi yao ya kiporo iliyochezwa uwanja wa taifa.
Goli la kwanza la Yanga lilipatikana kwa mkwaju wa penati baada ya beki wa Ruvu Shooting kuushika mpira akiwa kwenye eneo la hatari. Mpigaji wa penati wa Yanga Simon Msuva akakwamisha mpira kambani na kuiandikia Yanga bao la kuongoza.
Jambo lililozua utata kwenye mchezo huo ni pale mwamuzi wa mchezo Ahmad Simba alipolikataa goli la Obrey Chirwa na kumuonesha kadi ya njano kwa madai alifunga goli hilo kwa mkono. Chirwa alifunga goli hilo kwa kichwa akiunganisha krosi ya Simon Msuva kutoka Kusini Magharibi ya uwanja.
Dakika chache baadaye, mwamuzi akamuonesha Chirwa kadi ya pili ya njano iliyosababisha kadi nyekundu kwa kuudundisha mpira akiashiria kutokubaliana na maamuzi ya refa aliyepuliza filimbi baada ya Chirwa kumfanyia faulo mchezaji wa Ruvu Shooting.
Kipindi cha pili Yanga wakiwa pungufu walipoteza nafasi kadhaa za kufunga lakini nafasi zitakazokumbukwa zaidi ni zile za Msuva na Tambwe.
Wakati mechi inaelekea ukingoni, Emanuel Martin aliyeingia akitokea benchi, aliifungia Yanga bao la pili na la ushindi kwa kichwa alipounganisha pasi ya Musuva na kumwacha golikipa wa Ruvu Shooting Bidii Hussein akiwa hoi baada ya kujaribu kuufuata mpira na kujigonga kwenye nguzo ya goli.
Yanga imefikisha pointi 52 pointi mbili nyuma ya Simba huku timu zote zikiwa zimeshacheza mechi 23 hadi sasa, Yanga inaendelea kusalia katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu Tanzania bara huku Simba wakiendelea kusalia vinara wa kwenye msimamo.

Mshambuliaji wa DR Congo kutocheza kwa wiki sita

Mshambuliaji wa klaby ya Hull City Dieumerci Mbokani kuliaHaki miliki ya pichaPA
Image captionMshambuliaji wa klaby ya Hull City Dieumerci Mbokani kulia
Mshambuliaji wa klabu ya Hull City Dieumerci Mbokani hatocheza kwa kipindi cha wiki sita baada ya kupata jeraha la paja.
Mshambuliaji huyo wa DR Congo mwenye umri wa miaka 31 ambaye yuko kwa mkopo katika klabu ya Dynamo Kiev alibadilishwa wakati wa sare ya 1-1 dhidi ya Burnley.
Hull pia imethibitisha kuwa jeraha la goti alilopata beki Harry Maguire wakati wa mechi dhidi ya Burnley sio baya sana zaidi ya ilivyodhaniwa.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 huenda akapona tayari kwa safari ya kueleka Leicester City siku ya Jumamosi

Leicester yazungumza na kocha Roy Hodgson

Aliyekuwa kocha wa Uingereza Roy Hodgson afanya mazungumzo na LeicesterHaki miliki ya pichaREX FEATURES
Image captionAliyekuwa kocha wa Uingereza Roy Hodgson afanya mazungumzo na Leicester
Klabu ya Uingereza ya Leicester imefanya mazungumzo na aliyekuwa kocha wa taifa la Uingereza Roy Hodgson kuhusu kurithi pengo lililoachwa na Claudio Ranieri aliyepigwa kalamu.
Hatahivyo inadaiwa kuwa Roy ni miongoni mwa mameneja waliofanya majadiliano na wakuu wa timu hiyo.
Na kaimu mkufunzi Craig Shakespeare huenda akaendelea kuifunza timu hiyo hadi mwisho wa msimu iwapo matokeo yataendelea kuimarika.
Ranieri alifutwa kazi mnamo tarehe 23 mwezi Februari ,miezi tisa baada ya kushinda taji la ligi na kikosi hicho.
Mechi ya kwanza chini ya usimamizi wa Shakespear ilitoa majibu ya ushindi wa 3-1 dhidi ya liverpool siku ya Jumatatu.
Beki Danny Simpson alisema kuwa Shakespeare ''ni kocha mzuri sana''.
Alisema: Alituambia kwa urahisi kile anachotaka kufanya , na ilikuwa rahisi .Tumefanya hivyo na tunatumai kwamba tutaendelea hivyo

Picha/Video: Alikiba apata mapokezi ya nguvu JK Nyerere Airport, atua na tuzo ya MTV EMA


Mashabiki wa muimbaji Alikiba wamejitokeza kwa wingi JK Nyerere Airport kumpokea mkali huyo wa Aje akitokea Afrika Kusini huku akiwa na tuzo yake na MTV EMA – Best African Act.

Alikiba akiwa na tuzo yake
Akiwa Afrika Kusini alifanya media tour pamoja na show katika kumbi mbalimbali nchini huyo.
Muimbaji huyo aliiwambia waandishi wa habari kuwa tour yake hiyo ilikuwa na mafanikio makubwa katika muziki wake.Angalia picha na video za tukio hilo.
Visit source:  

Mshambuliaji wa DR Congo kutocheza kwa wiki sita

Mshambuliaji wa klaby ya Hull City Dieumerci Mbokani kuliaHaki miliki ya pichaPA
Image captionMshambuliaji wa klaby ya Hull City Dieumerci Mbokani kulia
Mshambuliaji wa klabu ya Hull City Dieumerci Mbokani hatocheza kwa kipindi cha wiki sita baada ya kupata jeraha la paja.
Mshambuliaji huyo wa DR Congo mwenye umri wa miaka 31 ambaye yuko kwa mkopo katika klabu ya Dynamo Kiev alibadilishwa wakati wa sare ya 1-1 dhidi ya Burnley.
Hull pia imethibitisha kuwa jeraha la goti alilopata beki Harry Maguire wakati wa mechi dhidi ya Burnley sio baya sana zaidi ya ilivyodhaniwa.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 huenda akapona tayari kwa safari ya kueleka Leicester City siku ya Jumamosi.

kweli steve nyerere anaishi kisaniii


Steve Mengere ‘Steve Nyerere’

WATU wengi walipigwa na butwaa na kubaki midomo wazi baada ya kuvuja kwa sauti inayodaiwa kuwa ni ya mchekeshaji Steve Mengere ‘Steve Nyerere’ na mama mzazi wa muigizaji Wema Sepetu.
Audio ilikuwa ya kawaida tu, lakini kilichofanya ionekane ishu, ni kule kuwahusisha watu wazito kwenye nchi hii na sakata la kukamatwa na baadaye kushtakiwa kwa matumizi ya bangi, kwa Wema. Kama ilivyotarajiwa, Steve Nyerere alitumia uungwana, akatoka mbele ya jamii na kuomba radhi.
Wasanii wa Bongo muvi katika kampeni ya Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu ‘Mama ongea na mwanao project’
Hicho ndicho kitu pekee ambacho alipaswa kukifanya, vinginevyo angekuwa mtu wa ajabu ‘kukausha’ ili kuacha upepo upite kama pepo zingine zinavyopita. Na niseme ukweli, utetezi wake pia nimeupenda, maana amesema kweli kuwa ilibidi atumie sanaa ili kumuweka vizuri mama ambaye aliishi naye vizuri kama mwanaye.
Ni vile tu mama Wema aliwahi kusema, lakini hata mimi nilikuwa najiuliza kwa kutomuona Steve akienda kumsabahi dada yake pale Central au hata kumsindikiza mahakamani. Historia inanionyesha huyu mchekeshaji huwa hakosi katika matukio yanayomhusisha Wema Sepetu na mara kadhaa, ameonekana akiwa karibu na mama Wema. Yes, ilibidi atumie sanaa ili kumuweka sawa na alifanikiwa.
Steve Nyerere wa kwanza (Kulia) katika mradi mwingine na wasanii/watu maarufu
Kwa hiyo, alichojaribu kusema ni kuwa yote aliyoongea ndani ya sauti ile, ni uongo. Kwamba hakwenda Dodoma, hakuongea na mawaziri waliotajwa wala wabunge na kwamba kilichotokea hakihusiani kwa namna yoyote na yeye. Lakini katika uhalisia wake, kuna uhusiano mkubwa wa kilichosikika na kilichotokea, ingawa siyo hoja ya leo hapa.
Ninachotaka tuwekane sawa, ni namna gani Steve Nyerere anapata mkate wake wa kila siku. Ukimsikiliza wakati akizungumza na waandishi wa habari, alisema yeye anaishi kwa sababu ya jina lake, alilotumia miaka mingi kulitengeneza. Steve ni muigizaji wa filamu na mchekeshaji. Huku kwenye filamu hajawahi kuwa staa wa kuuza sana kiasi cha kusema anaishi maisha tunayomuona kwa sababu hiyo.
Lakini pia kwenye uchekeshaji, siku hizi kuna kitu kinaitwa Stand Up Comedy, ile ambayo msanii anawajaza watu ukumbini na yeye kuanza kuwachekesha. Wanafanya hivi pia waigizaji wengine ambao kwa Afrika Mashariki, kinara wao ni Eric Omondi wa Kenya, Anna Kasiime wa Uganda na hapa nyumbani, MC Pilipili pia hufanya. Siku hizi Steve Nyerere naye anafanya Stand Up Comedy.
Steve Nyerere
Ni kwa kiasi gani Stand Up Comedy ya Steve inamuingizia hela ni jambo la kujadili. Steve anaishi sababu ya jina lake kwa kufanya kazi za sanaa au anaishi kisanii? Kuna uwezekano mkubwa pia kwamba licha ya sanaa, Steve anaishi kisanii, ndiyo maana sanaa aliyosema aliitumia katika kumuweka sawa mama Wema, inafanana sana na maisha yake halisi.
Steve anafika sehemu ambazo wengi hawawezi kufika na anazungumza na watu ambao siyo kila msanii anaweza kuwafikia. Watu wote waliotajwa katika ile sauti wanaweza kufikiwa na huyu msanii bila matatizo yoyote, ingawa zipo pia chumvi za kutosha katika hilo.
Unashangaa kumuona Steve Nyerere akipanda katika jukwaa la muziki na kuanza kumtunza mwimbaji manoti mengi mithili ya wale mapedeshee tuliowazoea, kina Chief Kiumbe, Papaa Msofe, Muzamir Katunzi, Jack Pemba, Ndama Mutoto ya Ng’ombe na wengine wa aina hiyo.
Kutoa ni moyo na si utajiri, lakini ni kweli kijana wa Kitanzania anayepata hela kwa jasho lake kihalali, anaweza kugawa fedha nyingi kwenye starehe kama Steve anavyofanya? Ingawa siungi mkono hata kidogo kitendo kilichofanywa na Mama Wema, ni vyema nikamtahadharisha Steve kwamba kilichotokea halikuwa jambo la bahati mbaya. Yale ndiyo maisha yake, ya kutumia sanaa yake.
Na huenda siyo kwa mama Wema pekee, sanaa hiyo yaweza kuwa imetumika ‘kuwaweka’ sawa pia watu kibao ambao hatuwafahamu!

hii ni maalum kwa wanaume wanaopenda six pack

  1. Majukumu na lifestyles zetu hua zinaweza kupelekea fat ikajikusanya mno tumboni na kupelekea kutokea kitambi au tumbo ambalo tunakua hatujaridhika nalo.
    Ikifika hatua hiyo tunachotakiwa ni kuiondoa hiyo fat hapo ilipo ili kupata lile tumbo ambalo litaridhisha macho yetu.

    Haya mazoezi yanaweza kufanywa kokote na jinsi zote wanaweza wakafanya.

    Jua kwamba.
    Kuna mazoezi mengi ya kupunguza tumbo, haya ni yale ambayo nayatumia mimi hivyo mengine yapo modified kwa kadri mimi ninavyoyafanya.

    Kisayansi six packs hazihesabiwi kama ni alama ya mtu kua ni mwenye afya, hii ni kwa kua unakua umeondoa fat yote tumboni ambayo tumbo lako huihitaji. But fvck science on this one.

    Na-assume sisi ni beginners, kama uko advanced ongeza idadi ya reps (30).

    Kanuni Yetu Ni Hii.
    -Kila zoezi litakua na seti tatu.
    -Kila seti moja itakua na reps 10 mpaka 12.
    -Kupumzika kati ya reps na reps ni sekunde 15.
    -Kupumzika kati ya zoezi na zoezi ni dakika moja.

    Tuanzeni...

    Kuendesha Tairi.
    9k%3D.jpg
    Utakua ukianza kwa kurudisha nyuma tairi na kukipeleka mbele kiasi mgongo wako unakua umenyooka. Ukipeleka mbele ukikirudisha hiyo ni moja.
    Kwa sisi ambao hatuna balansi, napendekeza upande tunaojinyoosha kuwe na kitu cha kutuzuia ili tusiende chini moja kwa moja mfano kukiwa na ukuta itakua vizuri zaidi.
    Hapa tunafanya reps 10 kwa seti tatu.

    Crunches.
    Unakua umelala chini magoti yameinuka, unaunyanyua mwili nusu, yaani sehemu ya kiuno inakua hauiinui.
    Sit_up_Crunch_M_WorkoutLabs.png
    Unakua unainuka lakini bila lengo la kuyafikia magoti yako. Ukinyanyuka na kurudi chini hiyo ni moja.
    Hapa tunafanya reps 12 mara tatu.

    Crunches Miguu Juu.
    Unakua umelala ila miguu inakua juu ya kitu, sehemu miguu itakayokaa isikufanye kuuinua mwili wako iwe adhabu mimi huwa naweka juu ya kitanda.
    Ukiwa gym unaweza chagua benchi la kuwekea miguu yako.
    200px-Crunches-2.png
    Kama utaweza kuinuka mpaka kuifuata miguu yako na kuishika itakua vizuri, kama hauwezi panda kiasi cha kiuno chako kisiwe kimelala chini. Kama bado hauwezi fanya kama ulivyotoka kufanya zoezi lililopita.
    Hapa tunafanya reps 10 mara tatu.

    Sit ups.
    Unakua umelala na miguu umeinyanyua, hapa utanyanyua mwili wako wote wakati unayafuata magot yako lakini wakati unarudi chini mwili usiguse chini, sehemu ya kiuno na mgongo kidogo ndiyo utakua unailaza sakafuni.
    img_20150410_163518.jpg
    Hapa kurelax hupatikana kutokana na ukali wa mbinuko wa magoti tuliouweka, mfano mbinuko wa kwenye hiyo picha kwa anayeanza ni mkali mno.
    Tunafanya reps 10 mara tatu.

    Sit Ups Nusu Nusu.
    Hizi nilizimodify kutokana na mahitaji yangu, hilo jina nimetunga hapa hapa (sorry).
    Inakua sawa na zoezi lililopita isipokuwa hapa tunanyanyua mwili na kuishia kati kisha tunarudi chini baada ya hapo tunaanzia pale kati tulipokua tunaishia na kuyafuata magoti.
    IMG_20170201_091400.jpg
    (Samahani sijui kuchora.)
    Hapa tunafanya za kutokea chini na kuishia kati reps 6 na kuanzia hapo kati kueleka magoti reps 6. Tutafanya hivyo mara tatu.

    Sit Ups Tatu kwa Moja.
    Hii ni nyingine ambayo niliimodify.
    Utalala chini kama kawaida ila Miguu yako utaitanua kiasi cha kuweza kuona mbele.
    1485932262367.jpg
    Utakua ukinyanyuka mikono yote unapeleka upande wa kushoto, unarudi chini.
    Ukinyanyuka tena mikono unapeleka upande wa kulia, unarudi chini.
    Ukinyanyuka mikono utapitisha kati kati ya miguu.
    Hiyo ni moja.
    Tutafanya hivi reps 3 mara tatu.

    Oblique Sit Ups.
    oblique-situp1.jpg
    Tunafanya kama zoezi lililopita, ila hapa utakua ukiinuka kuyafuat magoti yako kiwiko cha mkono wa kulia kitakua kinaenda upande wa goti la kushoto na kiwiko cha upande wa kushoto kitakua kinaenda upande wa goti la kulia.
    Mfano, Utakua unanyanyuka kiwiko cha kulia kitaenda upande wa kushoto, utarudi chini, utanyanyuka tena kiwiko cha kushoto kitaenda upande wa kulia, utarudi chini. Hiyo ni moja.
    Tutafanya reps 7 kwa seti tatu.

    NB.
    -Jiandae kwa Maumivu ya tumbo na kuharisha kwa siku moja au mbili.
    -Kama una kitambi kikubwa sana napendekeza main dish ya zoezi lako iwe ni kukimbia mpaka baada ya muda, pia anza na zoezi la 1, 2, na 3 mengine utayaongeza polepole kadri utakavyokua unaendelea.
    -Mapendekezo yangu ya reps na seti unaweza ukapunguza au ukaongeza kulingana na mahitaji yako na uzoefu wako.
    -Natumia uzoefu na kujifunza kwa wengine, sijasomea, ushauri wangu siyo wa kidaktari.

Ads Inside Post