Jumatano, 1 Machi 2017

UGANDA : Mwanamume azikwa na dola 5,700 akamhonge Mungu asimpe hukumu kali siku ya kiyama

[​IMG]Mutumishi wa umma alizikwa na zaidi ya Sh200 milioni za Uganda (Sh5.7 milioni za Kenya) ili akamhonge Mungu asipewe hukumu kali atakapokutana na muumba wake 

Bw. Charles Obong mwenye umri wa miaka 52 aliyefanya kazi katika Wizara ya Utumishi wa Umma tangu 2006 hadi 2016, alisemekana alichanga pesa hizo na kuzihifadhi kwa minajili hiyo alipokuwa hai 

Alifariki Desemba 17 mwaka uliopita baada ya kuugua kwa muda mrefu akazikwa bomani kwake katika kijiji cha Adag-ani, Kaunti ndogo ya Aromo ilivyo wilayani Lira mkesha wa krismasi 

Alizikwa kwa jeneza la chuma linalokadiriwa kugharibu Sh 20 milioni za Uganda 

Shemeji yake, Bw David Elic alisema marehemu aliacha wosia na kusema atakapofariki, mke wake Bi. Margaret Obong aweke kiasi kikubwa cha pesa ya jeneza lake 

Alipanga kupeleka pesa hizo kwa Mungu ili amsamehe dhambi zake na kumwepusha kwenda kuteketea jahannamu bali apate uzima wa milele 

Ilisemekana alimwambia kaka yake, Bw. Justin Ngole na dadake, Bi Hellen Aber wawe mashahidi kuhakikisha mke wake atatimiza agizo hilo lake kikamilifu 

Wizara alimofanya kazi ni miongoni mwa zinazokumbwa na sakata kubwa za ufisadi nchini humo mabilioni ya pesa zimewahi kupotelea mifukoni mwa watumishi wa umma 

Hata hivyo, Mzee wa ukoo wa Okaba Bw Mike Gulu aliagiza mwili ufukuliwe wiki iliyopita na pesa hizo zikatolewa na kuhifadhiwa kwingine kwa sababu kulingana naye, ni mwiko kuzika watu na pesa pamoja na jeneza.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Ads Inside Post