Mei 10 2016 Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa limewasilisha hotuba yake ya mapitio ya makadirio ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka 2016/2017 ambayo imesomwa na Waziri wake Hussein Mwinyiambaye amesema…
>‘Wizara yangu inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kupatiwa kiwango pungufu cha fedha ikilinganishwa na mahitaji halisi ambayo ni makubwa’
‘Hali ya kutengewa bajeti ndogo na fedha pungufu imekuwa ikiathiri utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya Jeshi na pia kusababisha ulimbikizaji wa madeni hususani ya kimkataba ambayo tumeingia na makampuni mbalimbali kwa ajili ya kuliwezesha Jeshi kizana na kivifaa’
‘Mpango wa utekelezaji wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa wa mwaka 2016/2017 umekusudia kuimarisah utekelezaji kazi na ufanisi wa Jeshi kulingana na Dira na Dhima ya Wizara’
‘Ili Wizara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa na Taasisi zake iweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo katika mwaka 2016/2017 naliomba Bunge liidhinishe jumla ya shilingi 1,736,530,000.00 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na matumizi mengine ‘
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni