Rapper Jay Z ameingia tena kwenye headlines baada ya kusemekana kuwa na mtoto wa nje ya ndoa. Mama mzazi wa kijana “Rymir Satterthwaite“mwenye umri wa miaka 22 anasema Jay Z alimpatia ujauzito zaidi ya miaka 20 iliyopita na anachohitaji ni mwanae kukutana na baba yake mzazi ambaye ni Jay Z.
Mama wa kijana huyo anasema hii sio mara ya kwanza yeye kuongelea swala hili kwani alishawahi kufungua kesi mwaka 2010 na kumtaka Jay Z afanye vipimo vya DNA ili kuhakikisha kuwa yule ni mwanae bila mafanikio yoyote.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni