ImageAFPImageDangote amewahi kutoa msaada awali kwa waathiriwa
Mtu tajiri zaidi Afrika Aliko Dangote ameahidi kutoa mamilioni ya pesa kusaidia waathiriwa wa mashambulio ya kundi la Boko Haram kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Ameahidi kutoa $10m (£7m) kuwasaidia waathiriwa hao.
Mfanyabiashara huyo ametoa tangazo hilo baada ya kuzuru kambi za watu ambao wamelazimika kutoroka makwao kutokana na mashambulio ya kundi hilo la Kiislamu.
Bw Dangote awali alikuwa ametoa dola milioni sita kama msaada kwa watu hao.
ImagebImageDangote alitembelea kambi za wakimbizi
Miaka ya nyuma, wafanyabiashara wa Nigeria wametuhumiwa kwa kutotimiza ahadi wanazotoa za kutoa pesa za kuwasaidia waathiriwa.
Lakini afisa wa serikali nchini humo ameambia BBC kwamba, kwa mujibu wa ufahamu wake, Bw Dangote daima amekuwa akitimiza ahadi zake kwa waathiriwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni