Jumanne, 10 Mei 2016

kiongozi islamic state auwawa


ImageAFPImageAbu Waheeb wakati mwingine alifahamika kama Shakir Waheeb

Jeshi la Marekani limesema mmoja wa viongozi wakuu wa kundi linalojiita Islamic State ameuawa kwenye shambulio la kutoka angani.

Msemaji wa Pentagon Peter Cook amesema Abu Waheeb, ambaye amekuwa afisa mkuu wa kijeshi wa Islamic State katika mkoa wa Anbar nchini Iraq aliuawa pamoja na watu wengine watatu baada ya gari lao kushambuliwa katika eneo la Rutba.

Marekani imesema kifo cha Abu Waheeb ni pigo kubwa kwa uongozi wa IS.

Wahib alizaliwa 1986 na alikuwa mwanafunzi wa zamani wa sayansi ya kompyuta ambaye alielezwa na mitandao inayofuatilia shughuli za Islamic State kama mtu ambaye nyota yake katika kundi hilo ilikuwa iking’aa.

Alikamatwa na wanajeshi wa Marekani nchini Iraq na kuhukumiwa kifo lakini akatoroka jela mwaka 2012.

Mwaka uliofuata, alishiriki katika mauaji ya kundi la madereva wa malori kutoka Syria yaliyokuwa yakipitia 

gaidi wa mexico kuhamishwa gereza

ImageAPImageEl ChapoJaji ameamua kwamba mlanguzi mkubwa wa madawa ya kulevya Joaquin 'El Chapo' Guzman anaweza kusafirishwa hadi Marekani.

El Chapo alikamatwa Januari baada ya kuwa mbioni kwa miezi sita baada ya kutoroka kupitia mtaro kutoka gereza alimokuwa.

Siku ya Jumapili maafisanchiniMexico walimhamisha El Chapo hadi katika gereza lililo karibu na mpaka na Marekani.

Hatua hiyo imetokana na wasiwasi wa usalama, na sio kiashiria cha kusafirishwa hadi Marekani, kwa mujibu wa maafisa wa Mexico.

Lakini sasa jaji wa Mexico anasema mlanguzi huyo anaweza kusafirishwa hadi Marekani anakokabiliwa na mashtaka.

Hatahivyo, uhamisho wowote huedna ukachukuwa muda.

Mawakili wa El Chapo tayari wamekata rufaa dhidi ya uamuzi huo wa kumsafirisha mteja wao na wizara ya mambo ya nje Mexico ina hadi siku 30 kuamua iwao kuidhinisha uhamisho huo u kuupinga.

Jumatatu, 9 Mei 2016

liverpool yaonyesha jezi zake mpya

Klabu ya Liverpool ya Uingereza imeamua kutoa rasmi jezi zao mpya ambazo tutegemee kuwaona wakizitumia katika mashindano mbalimbali msimu ujao ikiwemo Ligi Kuu Uingereza, baadhi ya mastaa wa Liverpoolwaliokuwepo katika utambulisho wa jezi hizo ni Jordan Henderson, Philippe Coutinho na Simon Mignolet. 

Imekuwa kawaida kwa vilabu vya Ulaya kubadilisha muundo wa jezi kila msimu ila rangi ya asili ya jezi zao inabaki palepale,Liverpool tayari wametuonesha jezi mpya za msimu na tegemea kuziona wakizitumia msimu wa 2016/2017.

mcheki hapa mtoto wa nje wa jayz mwenye miaka 22+video coppyright


Rapper Jay Z ameingia tena kwenye headlines baada ya kusemekana kuwa na mtoto wa nje ya ndoa. Mama mzazi wa  kijana “Rymir Satterthwaite“mwenye umri wa miaka 22 anasema Jay Z alimpatia ujauzito zaidi ya miaka 20 iliyopita na anachohitaji ni mwanae kukutana na baba yake mzazi ambaye ni Jay Z.

Mama wa kijana huyo anasema hii sio mara ya kwanza yeye kuongelea swala hili kwani alishawahi kufungua kesi mwaka 2010 na kumtaka Jay Z afanye vipimo vya DNA ili kuhakikisha kuwa yule ni mwanae bila mafanikio yoyote.

waziri anaswa na kamera akipiga punyeto ofisini

Aibu Kubwa imekumkuta Waziri wa Mawasiliano wa Congo Baada ya kunaswa na Kamera ya Webcam akijichukua ofisini..Nyeti zinasema kuwa Waziri huyo alikuwa anafanya Webcam na Demu wake ambae alikuwa anamrekodi bila waziri kujua......Baada ya siku kadhaa video ikavuja....Video ni mbaya nimeshindwa kuiweka hapa..ila habari zilizotufukia ni kuwa waziri huyo amefutwa kazi kwa kitendo hicho cha aibu...

majina ya vigogo waliohifadhi fedha nje hadharani

Panama Papers: Majina ya Watanzania Waliohifadhi Fedha Nje ya Nchi yatajwa

Kwa wale waliokuwa wansubiri kupekuwa kwenye database ya Panama papers kuona kama kuna vijogoo wa Afrika hususani Tanzania wameficha fedha wanaweza kupekuwa sasa. Kila kitu kimewekwa online.

Baadhi ya majina ni;

Hasnain Ahmed Hassanali Tanzania, United Republic of Panama Papers

Mohamedraza Ahmed Hassanali Tanzania, United Republic of Panama Papers

Ahmedirfan Mohamedraza Hassanali Tanzania, United Republic of Panama Papers

MR. KASBIAN NURIEL CHIRICH Tanzania, United Republic of Panama Papers

Mr. Azizi ROSTAM Tanzania, United Republic of Panama Papers

Nawshad Ahmed Hassanali Tanzania, United Republic of Panama Papers

JORGE MARITINO Tanzania, United Republic of Panama Papers

EDUARDO MARTINO Tanzania, United Republic of Panama Papers

JORGE MARTINO Tanzania, United Republic of Panama Papers

EDUARDO MARITINO Tanzania, United Republic of Panama Papers

JACEK MONLNIK ROGOYSKI Tanzania, United Republic of Panama Papers

BOULDER MINING LIMITED Tanzania, United Republic of Panama Papers

MRS. SUKAINA MANJI Tanzania, United Republic of Panama Papers

Talal Mohamed Abood Tanzania, United Republic of Panama Papers

Abbas Mohammed Jessa Tanzania, United Republic of Panama Papers

NARENDRA VAGHJIBHAI PATEL Tanzania, United Republic of Panama Papers

Ms. Zuzana Kovacicova Tanzania, United Republic of Panama Papers

Mr. Eric PASANISI Tanzania, United Republic of Panama Papers

SAJJAD MOHAMEDHUSSEIN VIRANI Tanzania, United Republic of Panama Papers

Mr. Eric PASANISI Tanzania, United Republic of Panama Papers

Mr. Suril Shah Tanzania, United Republic of Panama Papers

Suril V. Shah Tanzania, United Republic of Panama Papers

Mr Kalpesh Menhta Tanzania, United Republic of Panama Papers

Roberta Thomaz de Mattos Brisolla Tanzania, United Republic of Panama Papers

NICHOLAS CHARLES WILSON Tanzania, United Republic of Panama Papers

SEYDOU KANE Tanzania, United Republic of Panama Papers

KONSEL JAMES WAMBURA Tanzania, United Republic of Panama Papers

Abbas Mohamed Jessa Tanzania, United Republic of Panama Papers

SUN MINING LIMITED Tanzania, United Republic of Panama Papers

Abdulaziz Mohamed Abood Tanzania, United Republic of Panama Papers

ABBAS MOHAMMED JESSA Tanzania, United Republic of Panama Papers

Mohamed Panju Jessa Tanzania, United Republic of Panama Papers

Abbas Mohamed Jessa Tanzania, United Republic of Panama Papers

HARIDATT VAGHJIBHAI PATEL Tanzania, United Republic of Panama Papers

Fauzi Mohamed Abood Tanzania, United Republic of Panama Papers

B.A. KOTECHA Tanzania, United Republic of Panama Papers

R.D. KOTECHA Tanzania, United Republic of Panama Papers

MRS. SUKAINA MANJI Tanzania, United Republic of Panama Papers

SUKAINA MANJI AND YUSUF MANJI AS TRUSTEES OF THE MANJI FAMILY TRUST Tanzania, United Republic of Panama Papers

ANIL VAGHJIBHAI PATEL Tanzania, United Republic of Panama Papers

Mrs Kantaben Manibhai Chhotabhai Patel Tanzania, United Republic of Panama Papers

MRS. ROSMINA KANANI Tanzania, United Republic of Panama Papers

MR. DANIEL LITTMAN Tanzania, United Republic of Panama Papers

Mrs. Aarti Puri Tanzania, United Republic of Panama Papers

Mr. Eric PASANISI Tanzania, United Republic of Panama Papers

Mr. Azizi ROSTAM Tanzania, United Republic of Panama Papers

Andre Schmid Tanzania, United Republic of Offshore Leaks

KANIZ MEHBUB MANJI Tanzania, United Republic of Offshore Leaks

Mr. Stuart Hugh MacDonald Tanzania, United Republic of Offshore Leaks

Mr Rameshchandra Chotalal Somani Tanzania, United Republic of Offshore Leaks

Rameshchandra C. Somani Tanzania, United Republic of Offshore Leaks

Mr. Rameshchandra C. Somani Tanzania, United Republic of Offshore Leaks

MEHBUB YUSUFALI MANJI Tanzania, United Republic of Offshore Leaks

Wengine ni;

LIERVAAG, M.Tanzania, United Republic ofPanama Papers

NICITERETSE, ROGERTanzania, United Republic ofPanama Papers

JAMES BABANTanzania, United Republic of, MauritiusPanama Papers

WHEELOCK HOLDINGS LTD. 26-NOV-1996 British Virgin Islands Tanzania, United Republic of Panama Papers

RICHMOND FINANCE CORPORATION 11-MAR-1986 Panama Tanzania, United Republic of Panama Papers

EXPRO ENERGY LTD. 23-JUL-2014 British Virgin Islands Tanzania, United Republic of Panama Papers

wachungaji wawili wa kanisa la kkkt wakamatwa kwa mauaji


Wakati mchungaji wa Kanisa la Moravian akikamatwa na meno ya tembo 11 ndani ya kanisa, huko Moshi wachungaji wawili wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za mauaji.

Tukio la wilayani Moshi, Mkoa wa Kilimanjaro linawahusisha wachungaji wawili wa KKKT, Rodrick Mlay (52) na Godbess Mamkwe (38) pamoja na wananchi watatu ambao jana walipanda kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mjini humo kwa madai ya kuua kwa kukusudia.

Wakati wachungaji hao wawili wakipanda kizimbani, Polisi mkoani Katavi kwa kushirikiana na askari wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi wanawashikilia watu wawili akiwamo mchungaji wa Kanisa la Moravian kwa tuhuma ya kunaswa wakiwa na meno ya tembo 11 wakiwa wameyahifadhi ndani ya kanisa.

Akizungumzia meno hayo, Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Damas Nyanda alisema watuhumiwa hao walikamatwa juzi katika Kanisa la Moravian lililopo Kijiji cha Usevya, Wilaya ya Mlele.

Nyanda alisema mchungaji huyo akiwa na mwenzake ambao wote majina yao yamehifadhiwa kwa sababu za upelelezi, walikamatwa kufuatia taarifa zilizolifikia jeshi hilo na askari wa hifadhi kuwa, watu hao wanajihusisha na biashara haramu ya meno ya tembo na wamekuwa wakiyahifadhi ndani ya kanisa.

Baada ya taarifa hizo, polisi na askari hao walifanya uchunguzi kuhusiana na taarifa hizo kwa kufika katika kanisa hilo na kufanya upekuzi uliofanikisha kukamatwa kwa meno hayo yakiwa yamehifadhiwa kwenye tenga la kubebea mizigo.

Kaimu kamanda huyo alisema katika matukio mengine mawili tofauti yaliyotokea Mei 8, saa mbili usiku kwenye maeneo ya Mgolokani, Kata ya Sitarike wilayani humo, polisi kwa kushirikiana na askari wa hifadhi hiyo walimkamata mtu mmoja akiwa na jino moja la tembo.

Nyanda alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa baada ya askari kufanya upekuzi ndani ya nyumba yake na kukamata jino hilo na lingine la simba.

Alisema wote waliokamatwa kwenye matukio hayo wanatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote ili kujibu tuhuma zinazowakabili.

Katika tukio la wachungaji waliofikishwa mahakamani mjini Moshi, Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Julieth Mawole alisema wakiwa na wananchi watatu aliowataja kwa majina ya Fadhili Mkenda (36), Jackson Ruben (45) na Mathayo Moses (27), Mei 4 katika eneo la Kilema Pofo wanadaiwa kumuua kwa makusudi Frank Peter (19).

Hakimu Mawole aliwataka watuhumiwa hao kutojibu lolote na kesi dhidi yao itasikilizwa Mei 23 katika Mahakama Kuu Kanda ya Moshi na wote walipelekwa rumande kwa sababu shtaka waliloshtakiwa nalo halina dhamana kisheria.

Katika hatua nyingine, raia wa Marekani, Mbaraka Mtambo (50) amekamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) akiwa na maganda mawili ya kobe bahari aliyokuwa ameyafichwa kwenye begi la nguo.

Kamanda wa Polisi wa JNIA, Martin Otieno alisema raia huyo mwenye asili ya Tanzania, alikamatwa juzi saa 3.45 usiku akijiandaa kwa ajili ya safari ya kwenda Marekani na ndege ya Shirika la KLM kupitia Uholanzi.

Ads Inside Post