Jumanne, 10 Mei 2016

nauli za kulipa daraja za kigamboni zipo hapa

Tayari Dar es salaam imeanza kufurahia urahisi wa kuvuka bahari kwa urahisi zaidi kwenye safari kati ya Kigamboni na Town Dar es salaam ambapo daraja lilivyozinduliwa tu tuliambiwa tutalipia ila hatukutajiwa bei, leo May 10 2016 ndio bei zimetajwa na unaweza kuzipata hapa chini.

Kaongea Injinia Joseph Nyamwuhanga kataja kila kitu >>> ‘Shughuli za kutoza fedha zitasimamiwa na shirika la NSSF na tumeweka tozo kwa watumiaji wa aina mbalimbali mfano Magari na Pikipiki na kila mmoja atalipa kulingana na aina ya chombo chake’

‘Kwa waendao kwa miguu wataendelea kupita bure mpaka Serikali itakapoweka utaratibu tofauti, wenye baiskeli tozo itakuwa shilingi 300/= ila kwa sasa watapita tu bure mpaka tutakapowatangazia siku ya kuanza kulipa, kwa wenye pikipiki watalipa shilingi 600/=, Baiskeli za miguu mitatu (Guta) watalipa shilingi 1500/=’  

‘Mikokoteni watalipa shilingi 1500/=, Pikipikiza Miguu mitatu ambazo ni Bajaji watalipa Tsh. 1500/=, Gari ndogo (Saloon Cars) watalipa kwa shilingi 1500/= Magari aina ya Pick-Upyasiyozidi tani mbili yatalipa shilingi 2000/=, (Minibuses) mabasi madogo yanayobeba abiria wasiozidi 15 yatalipa shilingi 3000/=,Mabasi yanayobeba abiria kati ya 15 -29 yatalipia Tsh. 5000/=, Tractor ni Tsh. 7000/= 

‘Tractor yenye trailer lake hao watalipa shilingi 10,000/=, Magari yenye uzito wa tani 2 mpaka 7 watalipia 7000/=, magari yenye uzito wa tani 7 mpaka 15 watalipia 10,000/=, magari yenye uzito wa tani 15 mpaka 20 watalipia 15,000/=, magari yenye tani  20 mpaka 30 watalipia shilingi 20,000/=, Semi  Trailer kama magari yanayobeba mafuta  yatalipia 30,000/=, Truck Trailer watalipia shilingi 30,000/=,

ajifungua mapacha watano

ImageWatoto Keith, Ali, Penelope, Tiffany na BeatrixMama mmoja raia wa Australia ametoa picha za mapacha watano aliowazaa mwezi Januari.

Kim Tucci wa miaka 26 alichukua dadika mbili tu kujifungua wanawe hao, wasichana wanne na mvulana mmoja.

Wote walitungwa kawaida, hakutumia matibabu yeyote ya uzazi.

ImageFamilia inasema watoto huvishwa vibinda 350 kwa wiki

Madaktari 50 walimsaidia mama huyo kujifungua kwa njiya ya upasuaji, na wanawe wote wako shwari.Wanasayansi wanasema ni mama mmoja kati ya milioni 55 ana nafasi ya kuzaa mapacha watano.

Bi Tucci alipata umaarufu sana wakati alipoweka taarifa za mimba yake katika ukurasa wake wa Facebook.Kampuni ya kunasa picha ya Erin Elizabeth imesaidia sana kunadi safari ya Bi Tucci wakati wa uja uzito wake.

ImageKim Tucci akiwa mja mzito na pacha wake

Mama huyo ameelezea changamoto alizokumbana nazo akisema kwa wakati mmoja alihisi kama anapoteza maisha.Ameongeza madaktari walimshauri kuwaokoa watoto wawili na kumtaka kuwatoa wengine kutokana na sababu za kiafya.

Hata hivyo aliamua kubeba mimba yake hadi mwisho.

Bi Tucci na mumewe bwana Vaughn wana watoto watatu mvulana na wasichana wawili.Wameanza kuchangisha pesa ili kununua gari kubwa ambalo litaweza kukimu familia hiyo kubwa.

amir khan sitapigana na kell brook

Amir Khan: Sitapigana na Kell Brook

ImageAFPImageAmir Khan

Bondia Amir Khan amesema hakuna uwezekano wowote wa yeye kuchuana na mpinzani wake mkuu Kell Brook, licha ya kushindwa vibaya na Saul Canelo Alvarez.

Kulikuwa na matumaini makubwa kuwa kufuatia uamuzi wake wa kujiunga katika uzani wa Kati au Middleweight, pigano kati yake na bingwa wa shirisho la kimataifa la dondi IBF, Kell Brook, lingeandaliwa.

Lakini Khan amesema Brook sio bondia mwenye tajiriba na kwa sasa hawezi kushiriki pigano lolote dhidi yake.

Amesema anamheshimu bondia huyo, kwa sababu ni bingwa wa dunia lakini tofauti zao haziwezi kumruhusu kukubali pigano lolote naye.

'' Ningependa kupambana na mabondia mashuhuri duniani, ili kuwa na rekodi nzuri na kwa sasa nimesalia na mapigano machache tu'' Alisema Khan.

ImageBondia Kell Brook

Khan anayetoka eneo la Bolton na Brook kutoka Sheffield wamekuwa wakitaniana kwa muda na wakati Brook aliposhinda taji la dunia pigano dhidi yao likionekana kukaribia.

Lakini baada ya kutokuwa na taji lolote la dunia, na kupoteza kwa mara ya nne tangu mwaka wa 2012, Khan anasema Brook sio bondia wa kiwango chake.

Khan mwenye umri wa miaka 29, huenda sasa anapimana nguvu na Mmarekani Danny Garcia, bingwa wa shirikisho la WBC, ambaye alimshinda kwa njia ya knockout miaka minne iliyopita.

mabasi ya mwendo kasi yaanza

ImageMabasi ya mwendo wa kasi TZ

Huduma ya mabasi ya uchukuzi yanayoenda kwa kasi BRT nchini Tanzania imeanza rasmi siku ya jumanne katika jiji la kibiashara la Dar es Salaam.

Abiria watalipa shilingi 400 na 800 huku wanafunzi wakilipa 200 kulingana na mamlaka ya uchukuzi wa barabarani na majini SUMATRA.

ImageKituo cha mabasi ya mwendo wa kasi Tanzania

Mkurugenzi mkuu anayesimamia mamlaka hiyo bw Giliard Ngewe amewaambia maripota mjini humo kwamba nauli zitakuwa shilingi 400 kwa uchukuzi wa barabara ndogo,650 kwa barabara kuu na shilingi 800 kwa uchukuzi wa barabara kuu na ndogo huku wanafunzi wakilipa shilingi 200 kwa kila safari.

ImageAbiria wakiwa wamepanda basi la BRT

ASiku ya Jummanne na Jumatano mabasi hayo yatahudumu kati ya saa kumi na moja alfajiri na saa sita mchana.

ImageKituo cha mabasi ya BRT Tanzania

Tunawaonya wanaoendesha pikipiki na madereva wa magari mengine kutotumia barabara za mradi wa BRT,alisema akiongezea kwamba bado wanazungumza na washikadau kutafuta njia nzuri ya kupanga barabara zitakazotumiwa na BRT na mabasi mengine ya abiria.

Kulingana na yeye,mfumo huo wa BRT hauyaruhusu mabasi mengine kutoa huduma pamoja na mabasi ya BRT kwa hivyo abiria walioko katika barabara za BRT hawataruhusiwa kutumia mabasi mengine.

Lipumba uhaba wa sukari umesababishwa na magufuli

Akihojiwa na Mtangazaji Yvonne Kamuntu kwenye Azam News, Mchumi mbobezi hapa nchini Prof. Ibrahim Haruna Lipumba amesema uhaba wa sukari uliopo kwa sasa nchini umesababishwa na Rais John Magufuli mwenyewe kwa kuzuia sukari ya nje kutoingizwa Nchini, ilhali viwanda vyetu havikidhi idadi inayohitajika katika uzalishaji wake.

Pia Prof. Lipumba amesema hakuna sheria inayoruhusu Serikali au Bodi ya Sukari kupanga bei ya sukari nchini hivyo ametaka siasa kuacha kutumika katika mambo serious na wafanyabiasahara wasitishwe.

mkuu wa wilaya ya kinondoni afanya tena safari y kushtukiza

May 10 2016 Mkuu wa wilaya ya kinondoni, Ally Hapi amefanya ziara ya kushtukiza asubuhi na mapema majira ya saa kumi na mbili  katika hospitali ya Sinza Palestina na kujionea changamoto zinazoikabili Hospitali hiyo.

Baadhi ya changamoto ambazo amezikuta Hospitalini hapo ni pamoja na wagonjwa kukosa neti kwenye vitanda, upungufu wa dawa na kukosekana kwa jenereta lenye nguvu la kuendeshea vifaa vinavyotumia umeme mwingi hivyo kushindwa kutoa huduma pindi umeme unapokatika.

Mkuu huyo wa wilaya anatarajia kukaa na uongozi wa Hospitali zote za serikali zilipo wilaya ya kinondoni kuona namna ya kutatua changamoto zinazowakabili.

.

Jenereta ambalo huwa linatumika pindi umeme unapokatika lakini halina nguvu ya kuendeshea vifaa vinavyotumia umeme mwingi hivyo kushindwa kutoa huduma.

Umeme wa Nishati ya jua ambao pia hauna nguvu ya kuendeshea vifaa vinavyotumia umeme mwingi hivyo kushindwa kutoa huduma pindi umeme unapokatika

.

.

.

.

.

.

.

.

.

polisi waandamana kisa beyonce

ImageGettyImageBeyonce Knowles

Kundi moja la maafisa wa polisi limefanya maandamano karibu na tamasha lililofanyika katika mji wa nyumbani wa nyota wa muziki Beyonce huko Houston.

Wanachama wa muungano wa polisi na Sherrif walisimama mbali na uwanja wa soka na kuelekeza mwangaza wa bluu katika ukumbi wa tamasha hilo.

Walikuwa wanapinga kanda ya video ya Beyonce ambayo wanasema inawaponza polisi.

ImageReutersImageMaafisa wa polisi wa Marekani

Mwanamuziki huyo tayari amesema kwamba hawakosoi polisi katika wimbo huo na kusema kuwa maafisa wa polisi wanaodhani aliwaponza wanakosea.

Mwanachama mmoja wa polisi amekiambia chombo cha habari KHOU11 kwamba hawakufurahia baada ya Beyonce kutumia picha za gari moja la polisi mjini New Orleans iliokuwa ikizama katikamafuriko.

''Tunaamini kwamba baadhi ya mambo yake ni kinyume na maafisa wa polisi'',alisema.

ImageBeyonce_black_Panther

Mnamo mwezi Aprili,Beyonce aliambia jarida la Elle kwamba anaheshimu polisi lakini hapendi unyanyasaji.

''Mtu yoyote anyedhani kwamba siwapendi polisi anakosa kwa sababu'', alisema.

''Ninawapenda na kuwaheshimu sana polisi pamoja na familia za maafisa hao ambao hujitolea ili kuhakikisha tuko salama''.

Ads Inside Post