Jumatano, 1 Machi 2017

mfahamu carlos gaidi namba moja duniani


Kama kazi yako imekushinda usiendelee kuniuliza maswali ya kitoto. Carlos alikemea kwa sauti kali huku akikuna ndevu zake ambazo tayari zilianza kuota mvi.
[​IMG]

Jaji wa mahakama kuu ya Ufaransa, Prof. Olivier Laurent akamwamuru kwa mara nyingine tena ajitambulishe kwa usahihi jina na kazi yake.

Mbweha (The jackal) kwanza akatabasamu kwa dharau ya wazi, akageuka kushoto kumtazama mwanasheria wake mama Isabelle Peyre (ambae baadae kidogo alikuja kumuoa na kuwa mkewe wa tatu), kisha akafungua kinywa chake akasema "Mimi ni muongeaji mzuri sana, ni jambo la kipuuzi ikiwa wewe jaji pamoja na mahakama yako tukufu mmeshindwa kuligundua hilo. Haina haja ya kuendelea kaniuliza mimi ni nani, zunguka ulimwengu mzima, uliza mimi ni nani, wananifahamu vizuri. Kuhusu swala la kazi yangu, hakuna mpumbavu japo mmoja asiyetambua kuwa mimi ni mtaalamu wa mapinduzi (professional revolutionist)".
[​IMG]
Carlos akiwa amezungukwa na askari siku ya hukumu yake.

Kwa mara nyingine tena ya tatu, Carlos alipatikana na hatia na kuhukumiwa kuozea jela.

Baada ya hukumu hii aliongea na mwandishi wa BBC kwa kufedheheka sana akasema "Ni muujiza nipo hai hata leo, Mungu ni mzuri sana, nimesalimika kuingia kuzimu katika mapambano mengi sana dhidi yangu, hata hili nalo halitanishinda. Naumia sana sijawahi kuwa baba mzuri kwa binti yangu Elba Rosa, wala mume mzuri kwa mke wangu. Kitu kinachoniuma zaidi rafiki yangu Raisi wa Venezuela Hugo Chavez hanitumii tena sigara tamu, siruhusiwi tena kuzungumza na wafungwa wenzangu. Naamini nikitoka jela nitakutana tena na Fidel Castro tugonge mvinyo wa ikulu"
[​IMG]
Hugo Chavez aliwahi kusema "Carlo is a distinguished compatriot"_ "Carlo ni jembe langu la uhakika"

Carlos the jackal ni nani?

Tarehe 12 Oct 1949 mwanasheria nguli wa Venezuela Jośe Ramiréz na mkewe Elba Maria walifanikiwa kupata mtoto wa kiume katika kitongoji maarufu cha Tachira. Bwana Jośe Ramurez alikuwa ni mtu aliyeshikilia mno msimamo na itikadi kali za Umaski (Marxism) hivyo aliwaita wanae wote watatu kwa ukumbusho wa kiongozi maarufu wa Urusi raisi Ilyich Lenin Vladimir aliyeshikilia haswa itikadi ya Umaski. Mwanae wa kwanza ambaye ndio Carlos alimuita Ilyich Sanchez Ramirez, mwanae wa pili Lenin na watatu Vladimir.

Kutokana na uwezo wa kifedha wa baba yake, Sanchez (Carlos) alibahatika kwenda shule mbali mbali zenye hadhi nzuri kielimu. Carlos hakupenda kabisa masomo ya kawaida, alipofika tu miaka 15 Sanchez aliamua kujiunga na vuguvugu la vijana wa chama cha kikomunisti cha Venezuela. Ambapo mara kadhaa walifanya fujo, maandamano na ghasia kupinga uongozi wa chama tawala.

Akiwa na miaka 17 baba'ke aliamua kuongozana nae kushiriki katika mkutano mkuu wa Umoja wa mabara matatu (tricontinental conference), mkutano uliohusisha mabara ya Africa, Asia na Amerika Kusini.

Kwa mara ya kwanza Sanchez alipata uhalisia wa jinsi dunia inaendeshwa ambapo aligundua kua nchi za bara la Ulaya na Marekani zilitumia resources zilizokua nazo kunyonya nchi za dunia ya tatu (3rd world countries).

Hapa ndipo sumu ya mapinduzi ilipoanzia. Mara baada ya mkutano wa umoja wa mabara matatu kuisha, Sanchez alimuomba baba yake ampeleke shule ya mafunzo ya kijeshi.

Jan 1966 akiwa amebakiza miezi kadhaa afikishe miaka 18 baba'ke aliamua kumpeleka chuo cha mafunzo ya vita vya porini (guerilla warfare) kinachoendeshwa na shirika la kijasusi la Cuba (Cuban DGI) nje kidogo ya mji mkuu wa Cuba, Havana.

Mwishoni mwa mwaka huo wazazi wake walitengana. Mama yake akaelekea London na watoto wote, ambako alikua akiendelea na masomo katika chuo cha Staffort. Mwaka 1968, Sanchez akiwa na miaka 19 alichukuliwa na babake akasome Paris, Ufaransa, lakini Sanchez aligoma kabisa na kupendekeza apelekwe chuo kikuu cha Patrice Lumumba kilichopo Moscow mji mkuu wa Urusi. Kwa mujibu wa BBC, chuo hiki kiliasisiwa kwa malengo ya kuandaa viongozi wenye misimamo mikali ya kikomunisti hasa wa nchi za dunia ya tatu. Chuo hiki kimepika viongozi wa juu wa nchi mbali mbali za Afrika ikiwemo Sudan, Namibia, Benin, Afrika ya kati nk.

Kutokana na tabia za ukorofi, fujo, utukutu, uhuni na kuishi kiPlayboy alichukiwa sana na wakufunzi. Mwaka 1969 Sanchez aliandaa maandamano ya wanafunzi wa kiarabu nchini hapo, kosa lililomfukuzisha chuoni hapo.
[​IMG]
Picha ya passport ya Carlos iliyopo kwenye vyeti na hati yake ya kusafiri.

Mwaka 1970 Sanchez alitimkia Palestine, ambapo alijiunga na kikundi maarufu sana miaka ya 70 kilichoitwa Chama Mashuhuri cha Ukombozi wa Palestine (Popular Front for Liberation of Palestine-PFLP). PFLP kilikua ni kikundi cha kigaidi kilichojificha chini ya mwamvuli wa multipartism, ambacho kilikuwa kikidhaminiwa na KGB (Taasisi ya Urusi ya Ulinzi na Ujasusi), kikundi hiki kilianzishwa mahsusi kwajili ya kuleta vurugu nchini Israel ili kudhoofisha usalama wa taifa hilo.

Akiwa PFLP Sanchez alipata mafunzo ya daraja la juu ya ugaidi, vita vya porini, silaha na mbinu za kijeshi. Sanchez alionesha uhodari mkubwa sana hasa katika shabaha, ukakamavu na kupika mipango ya uvamizi na utekaji.

Sept mwaka huo Kikundi cha shirika la ukombozi wa Palestine (Palestine Liberation Organisation) chini ya Yasser Arafat kiliingia mgogoro na jeshi la nchi ya Jordan, hivyo kuibuka vita maarufu iliyopewa jina la September nyeusi (Black September). Chama cha PLO kilipozidiwa nguvu baada ya mapambano kikaomba msaada wa kijeshi kutoka kwa kikundi cha kina Sanchez, PFLP.

Akiwa kijana mdogo kabisa wa miaka 21 aliteuliwa kuongoza kikundi cha PFLP kipambana vita ya Black September. Bwana mdogo alibadili kabisa upepo wa vita hiyo, jeshi la Jordan liligaragazwa vibaya mno, Sanchez alichora mbinu za uvamizi zilizowachanganya maadui. Alibuni magwanda ambayo yalifanana sana na yale ya jeshi la Jordan, akachora ramani ya kutengenga mitaro ya chini kwa chini (tunnels) kutoka walipoweka kambi hadi walipo jeshi la Jordan, walifika eneo la tukio usiku na kisha kujichanganya na wanajeshi wa Jordan. Baada ya hapo mashambulizi yanaanza.

Mbinu hii ilifanikiwa sana mpaka Mfalme wa Jordan Hussein akaomba maridhiano. Bado Sanchez hakuridhika, akasuka ramani za kuteka ndege zilizotua Jordan. Mwezi huo huo September alifanikisha utekaji wa ndege nne zilizotua Jorsani zikiwemo SwissAir, TWA , Azraq na BOAC. 

Uhodari katika vita hii ya black September ndio ulimfanya Sanchez abatizwe jina la Carlos, ambalo ni maarufu nchi za Amerika Kusini kumaanisha 'Mwanaume shujaa'

Kiongozi mkuu wa PFLP Generali Wadie Haddad alifurahishwa na umakini wa Carlos hivyo kuamua kumpeleka London akapate mafunzo ya juu zaidi ya kijeshi. Mwaka uliofuata 1971 Carlos alienda mafunzoni London na ndipo alianza matukio ya kigaidi.

Bingwa wa mission impossible katika karne ya 20.

Akiwa Uingereza 1971, alipanga nyumba ya kawaida nje kidogo ya jiji la London, alitumia miezi minne kubuni na kufunga systems za usalama kwajili ya ulinzi wa nyumba yake. Kutendo hiko kilipelekea askari kumtilia mashaka. Polisi kadhaa walifika nyumbani kwake kufanya upelelezi ili kufahamu nini hasa Carlos anakusudia. (Ikumbukwe kua jina la Carlos lilikua maarufu sana lakini hakuna aliyemtambua kwa sura). Baada ya upelelezi, polisi hawakufanikiwa kumkuta na kosa lolote.

● 26 Oct 1972, Carlos alifoji passport ya Costa Rica na kutoka Uingereza kuelekea Damascus mji mkuu wa Syria. Alifanya hivyo kuwachanganya polisi, yani documents zioneshe bado yupo Uingereza wakati yupo Syria. Tarehe 27 na 28 akasuka ramani ya utekaji, akawaandaa wenzake wawili. Tarehe 29 wakaingia uwanja wa ndege wa Damascus, saa 6 mchana ndege ya Lufthansa (Boeing 727-100) iliyokua inaelekea Frankfurt, Ujerumani ikatekwa nyara.

Carlos akatuma salamu kwa raisi wa ujerumani kupitia Waziri wa ulinzi Dr. Theodore Blank. Serikali ikamwomba sana Carlos awaache mateka wakiwa salama kwa gharama yoyote ile. Carlos akamwamuru kua kila mateka matatu ni sawa na mfungwa mmoja wa PFLP aliyefungwa Ujerumani hivyo anataka wafungwa waachwe huru. Makubaliano yakafikiwa kwa pande zote mbili.

Carlos akamwamuru rubani apaishe ndege kuelekea Zagreb, Croatia. Mateka wote wakashushwa wakiwa salama kisha ndege ikarushwa hadi Tripoli, Libya. Carlos na wenzake wakapewa hifadhi na Gadaffi. Keshowe tarehe 30 Carlos akarudi zake London.

● Siku 3 baadae mashindano ya Olympics yalianza nchini Ujerumani. Kundi la Black September lilimuomba Carlos awasaidie kutekeleza shambulio litakalopeleka ujumbe kwa dunia kuhusu unyonywaji wa taifa la Palestine. Carlos aliunda shambulio hatari ambalo leo hii ni maarufu kwa jina la mauaji ya Munich (Munich Massacre). Lakini Carlos hakutaka kushiriki kwenye shambulio hilo, alikaa pembeni.

Tarehe 5 Sept wanaOlympic 11 wa Israel walitekwa na kuuwawa na Black September. Wote waliohusika na mauaji hayo waliteketezwa mmoja baada ya mwingine kwa nyakati tofauti na shirika la ujasusi la Israel, MOSSAD. Lakini Carlos alibaki anadunda tu London.

Taarifa za siri zilizovijishwa na WikiLeaks zinadai kwamba MOSSAD hawakuweza kumuuwa Carlos kwamba hakuwa na hajawahi kuwa tishio kwao.

● Bado akiwa mafunzoni London, Nov mwaka huo huo Carlos alipiga tukio la kushtukiza ambapo katika siku 1 kulikua na uvamizi wa mabomu katika benki ya Israel tawi la London na kituo cha gazeti 1 maarufu la Israel. Magari na majengo yaliharibika lakini hakukuripotiwa vifo wala majeruhi. Baada ya shambulio hiyo ndipo Carlos aliingia rasmi kwenye ligi la wababe Ulaya, akateka rasmi attention ya vyombo vya ulinzi na usalama.

● Dec 30 1973, Carlos aliamka mapema kabisa, akafungua briefcase, akashika mafuta na kitambaa akasafisha pisto yake aina ya Tokaruv, kisha akahesabu risasi 4 akazitia kwenye magazine. Akachukua sigara akavuta vipisi viwili kisha safari ya kuelekea nyumbani kwa Josef Sieff ikaanza. 

Josef Sieff alikua mfanyabiashara mkubwa Uingereza mwenye damu ya kiyahudi na pia alikuwa mwenyekiti wa shirikisho la kizayuni la Uingereza (British Zionist Federation), huyu jamaa mara kadhaa alitoa matamko ya kulaani viongozi, vyama vya ukombozi na wananchi wa Palestine. 

Alipofika alikua na kibali cha kufoji kilichomwezesha kuruhisiwa na walinzi kuingia. Baada ya kuingia ndani alikutana na binti wa kazi wa Josef, akamuomba aoneshwe alipo Josef. Alimkuta Josef akiwa bafuni anaoga, alichokifanya ni kuchuchumaa na kuchomoa pisto yake aliyoificha kwenye soksi, akachukua target na kuachia risasi moja ambayo alienda moja kwa moja usoni mwa Josef, bahati mbaya/nzuri ilimpunyua kati ya pua mdomo (upper lip). Carlos akajaribu kuvuta risasi ya pili bahati nzuri/mbaya akashtuka risasi zimejam kwenye silaha. Bila kupoteza muda akatoroka haraka sana na kumwacha Josef mahututi.
[​IMG]
Nyumba ya Josef 

Keshowe taarifa zilisambaa zikimuonesha kiongozi wa muda wa PFLP akisisitiza kuwa shambulio hilo ni kulipa kisasi kwa Israeli baada ya MOSSAD kumuuwa kiongozi mmoja wa juu wa PFLP Mohammed Boudia.
[​IMG]
Baada ya tukio hilo Carlos akakimbia London na kuelekea Palestine. 

● Shambulio lililofuata halikuwa rahisi. Mpango ulikuwa ni kulipua kwa kombora (rocket-propelled grenade) ndege 2 za israel za El Al zilizokua zikitua uwanja wa Orly karibu na Paris. Mashambulio haya yalifanyika kati ya tarehe 13 na 15. 

Mashambulio haya hayakufanikiwa kama ilivyopangwa, yalisababisha uharibifu wa ndege bila kifo wala majeruhi. Mbaya zaidi, gaidi mwenza wa Carlos Michel Moukharbal alikamatwa na askari wa Ufaransa katika tukio hilo.

Akiwa katika uangalizi mkali alihojiwa kwa kuteswa (enhanced interrogation), hadi alipofunguka na kutoa utambulisho wa Sura, muonekano na tabia ya Carlos ili kufanikisha kukamatwa kwake. Mourkharbal alikubali kushirikiana na kitengo cha ujasusi- DST cha kupambana na magaidi (counterterrorism) ili kufanikisha kukamatwa kwa Carlos. 

Moukharbal na maafisa wawili wa Ufaransa walifika nyumbani kwa Carlos. Carlos akiwa chumbani kwake aliwaona vizuri sana kupitia camera za ulinzi, akawapa kibali walinzi wawaruhusu kuingia. Carlos akakutana nao, wakasalimiana vizuri na kuwakaribisha kukaa. Carlos akanyanyuka akawapa juisi na stori zikaendelea.

Walivyomaliza kunywa Carlos akanyanyuka akamwambia Moukharbal, ni salama ukafia mikononi mwangu kuliko kuuwawa na nguruwe wa ulaya, akachomoa bastola akaanza kumuuwa Moukharbal kisha akawamalizia wale majasusi wa Ufaransa kisha akatoroka haraka kuelekea Beirut kupitia Brussels.

Tukio hili lilizagaa dunia nzima, ndipo vyombo vya habari vikambatiza jina la Mbweha (Tha jackal) na kumfanya awe tofauti na Carlos wengine wote duniani.

OPEC siege: Shambulizi la utekaji maarufu zaidi duniani.

Akiwa Beirut ndipo Carlos alishinda usiku na mchana kusuka mission ambayo aliamini vizazi na vizazi havitamsahau, mpango mzima ulikuwa ni kuyaliza mataifa makubwa yanayochimba na kusafirisha mafuta ambapo ndani yake kuna unyonyaji mkubwa kwa mataita madogo.

Ilikuwa hivi...
Jumapili ya tarehe kama ya jana Dec 21 1975 mjini Vienna kulikuwa na mkutano wa mwaka wa Jumuiya ya nchi zinazozalisha na kusambaza mafuta (Organisation for Petroleum Exporting Countries-OPEC). Mkutano huu ulihudhuriwa na Viongozi wakubwa wa mataifa mbali mbali.
[​IMG]
Mkutano wa OPEC 1975

Carlos akiwakilisha kikundi cha PFLP aliongoza timu ya watu 6 hatari katika uvamizi ulioushangaza ulimwengu akiwemo mwanamama nguli Gabrielle Kröcher (huyu alikuwa mwanamke wa kijerumani aliyeheshimika kwa kulenga shabaha kutumia mkono wake wa kushoto) .
[​IMG]
Mwanamama Gabrielle Krocher

Asubuhi saa 3 walifika makao makuu ya OPEC ambapo mkutano ulikua unaendelea. Askari wa 4 wa Australia walichangamkiwa mapema sana baada ya kina Carlos kuingia getini, mmoja wa askari hao alifariki papo hapo. Baada ya kuingia ndani, kabla mwajiri mmoja wa OPEC hajabonyeza simu kuwapigia askari, mwanamama Gabrielle alimtuliza kwa shaba 1 ya bega, hapo pia alijitokeza askari mlinzi wa Waziri wa mafuta wa Libya, naye aliwahiwa kabla hajaketa madhara, hivyo kufanya idadi ya vifo kufika watu wa 3.

Kina Carlos wakapata access ya kuingia kwenye chumba cha mkutano kilichokuwa na wajumbe 63 wakiwemo mawaziri 11 wa mafuta wa nchi mbali mbali. 

Carlos alichomoa simu ya waziri mmoja wa Austaria, akampigia raisi kumpa taarifa. Carlos alitoa masharti maraisi sana kwa serikali;-

》》Alitaka liletwe basi litakalowabeba mateka wote kuelekea Airport. 

》》Alitaka ndege iwepo pindi wakatakapofika airport na iwe full tanked.

》》Alitaka malalamiko yote ya Palestina dhidi ya mataifa mengine yarushwe kwenye televisheni na redio ya taifa ya Australia kila baada ya masaa ma 2.

La sivyo Carlos aliahidi kuuwa mateka mmoja baada ya mwingine kila baada ya dakika 15.

Australia walifahamu vizuri jinsi Carlos alivyo mtata na mwenye uwezo wa kukamilisha matukio kwa weledi mkubwa bila kuacha ushahidi wowote. Hivyo waliamua moja kwa moja kukubali matakwa yote ya Carlos pasipo pingamizi. 

Basi lililetwa mara moja, mateka wote na kina Carlos walielekea airport.
[​IMG]
Mateka wakielekea uwanja wa ndege.

Keshowe siku kama ya leo tarehe 22, walipewa ndege ya serikali aina ya Boeing, pia Carlos aliamrisha apewe rubani Neville Atkinson. Huyu alikuwa rubani mstaafu wa jeshi la anga la uingereza (royal navy pilot), wakati huo rubani huyo alikua rubani wa Kanali Muamar Gaddafi.
[​IMG]
Ndege iliyotumika kusafirisha mateka wa uvamizi wa OPEC

Carlos alimwamuru rubani apaishe ndege kuelekea Algiers, Algeria ambapo aliwaacha huru mateka 20 kwa makubaliano ya kupewa silaha, risasi, pamoja na kujazwa mafuta kwenye ndege. Baada ya hapo alimwamuru rubani apae kuelekea Tripoli.

Baada ya kufika Tripoli Carlos aliwaachia huru mateka 10 kwa makubaliano ya kubadilishiwa ndege apewe ya kifahari zaidi na yenye uwezo mkubwa na pia kuhakikishiwa ulinzi siku nzima kabla hajaondoka.

Tarehe 23 Dec kina Carlos na mateka waliwasiri tena Algiers ambapo aliahidi kuwaachia hai mateka wote iwapo atapewa kiasi cha pesa kisichopungua $50 mil na ahakikishiwe kupalewa hifadhi/maficho (asylum). Ilikuja kugundulika kuwa pesa hii ilitolewa na serikali ya Saudi Arabia na Iran na kwamba Carlos alitumia pesa yote akiwapa wenzake kiasi kidogo sana. Mateka waliachiwa huru baada ya Carlos kujiridhisha kua atapewa ulinzi wa kutosha hapo Algeria.

Hakuna kitu kilichomkera kiongozi mkuu wa PFLP kama shambulio la OPEC. Kwake yeye utekaji huo haukuwa na faidi yoyote kwani lengo walilopanga halikutimia. Kazi kina Carlos waliagizwa kuifanya ilikuwa ni kuwauwa mawaziri wa mafuta wa Saudi Arabia, Ahmadi na Jamshid wa iran. Pia Waddi Haddad alikerwa na kitendo cha Carlos kuchukua pesa zote kwa matumizi binafsi. Hivyo, Haddad ambae pia alikuwa mkufunzi wa Carlos wa maswala ya kijajusi aliamua kumtimua Carlos kutoka PFLP.

Hali ya usalama haikuwa nzuri kwa Carloa baada ya kutimuliwa PFLP, akatorokea Yemen Kusini, kisha akaelekea Libya alipopokelewa na kupewa hifadhi na Gaddafi, ambaye inaaminika ndiye alifadhili shambulio la OPEC (The Libyan Revolution: Its Origins and Legacy : a Memoir and Assessment). Akiwa Libya alijitolea kutoa mafunzo ya mbinu za vita vya porini (guerrilla warfare) kwa wanajeshi wa Jibya.

July 4 1976 ndege ya Ufaransa ilitekwa ikitokea Tel Aviv na kupelekwa Entebbe Uganda, taarifa zilisambaa kila sehemu kua mtekaji ni Carlos japo Carlos mwenyewe alipinga kuhusika na shambulio hilo.

Mwaka 1976 raisi mkorofi wa Iran Mohammad Reza Shah Pahlavi ambaye baadae alipinduliwa na Ayatollah alipata taarifa za kiintelijensia kuwa target kuu ya Shambulio la OPEC lilikuwa ni kumuuwa Waziri wake, hivyo alikasirishwa na kupania kumuuwa Carlos. Alitumia kiasi kikubwa sana cha pesa kuwakodi wauaji hatari wanne wamuondoe Carlos kwenye uso wa dunia. Magaidi hao walikuwa ni:-

>>Manuel Contreras: Huyu alikuwa afisa wa jeshi la Chile na mkurugenzi wa taasisi ya Intelijensia ya Chile (DINA). Huyu jamaa alifariki mwaka jana, akiwa anatumikia vifungo tofauti 59 visivyo na dhamana ambavyo vina hukumu ya miaka 529 kwa ujumla.
[​IMG]

>>Garhard Mertins: huyu ni Mjerumani mtaalamu wa kuruka angani kutokea kwenye ndege za kivita (paratrooper). Huyu jamaa ndiye alikua kiongozi wa operesheni Gran Sasso, shambulio lililomtorosha Benito Musolini kutoma gereza mwaka 1943.
[​IMG]

>>Sergio Arredondo: huyu jamaa katika naisha yake aliuwa watu 75 kwa mkono wake. Alikuwa kamanda msaidizi wa kikosi cha 'msafara wa kifo' (caravan of death).
Muuwaji wa nne hakuwahi kufahamika lakini inasemekana alikuwa ni Mpalestina.

Hawa wauaji wote kwa pamoja walipanga mashambulizi manne ya kumuuwa Carlos kutekeleza amri ya Shah Reza. Katika mission zao hawakuwahi hata siku moja kumuona Carlos japo taarifa za Carlos zote walikuwa nazo. Mwishowe waliamua kunyoosha mikono juu, wakarudisha mrejesho kwa Shah Reza kua kumuuwa Carlos ni sawa na kupaka rangi upepo.

Viongozi wa juu wa Stasi-Kitengo cha siri cha polisi cha Ujerumani Mashariki, walizikubali harakati za Carlos kwa muda mrefu, baada ya kupata taarifa kuwa hayupo salama, Nov 1976 walijitolea kumpa Carlos hifadhi ya nyumba za kifahari, ofisi kwajili ya kuanzisha kikundi chake kipya, magari pamoja na makomando wa kumpa ulinzi. Jambo la kushangaza zaidi ni kua Carlos aliruhusiwa kutembea na bastola hadi mtaani.

Mwaka 1977 Carlos alianza kuunda kundi lake la kigaidi liitwalo Arab Armed Struggle. March 1978 kiongozi wa PFLP aliuwawa kwa sumu aliyepuliziwa na MOSSAD, Carlos aliwashawishi wanamgambo wa PFLP wajiunge na kundi lake, jambo ambalo halikuwa na utata.

Mwaka 1979 Carlos alifunga ndoa na binti mkali kabisa wa Ujerumani Magdalene Kopp, ambaye pia alikuwa gaidi wa level ya juu sana.
[​IMG]

Carlos arejea tena kwenye ligi la wakubwa.

Bado Carlos hakuridhika kabisa na vyote alivyofanya, alihisi hajamaliza kazi iliyomleta duniani. Mwaka 1981 kupitia kikundi chake alirudisha mashambulizi kwa maadui zake wa Ulaya.

Kwanza alianza kuteka makao makuu ya Radio Free Europe yaliyopo Munich. Hakusababisha vifo lakini aliuamsha ulimwengu na kutoa ujumbe kuwa amerudi ulingoni.

Carlos alipata taarifa kua adui yake mkubwa Ufaransa anasuka vinu vya nyuklia. January 1982 alipanga shambulio la kulipua vinu vyote vya nyuklia vya Ufaransa. Katika uvamizi huo mipango haikwenda kama ilivyokusudiwa kutokana na ulinzi mzito uliokua maeneo hayo, hivyo kusababisha mke wa Carlos Magdalene kukamatwa akiwa na gari limejaa mabomu.

Carlos alituma barua ya kutaka Ufaransa wamwache huru mkewe, lakini Ufaransa hawakuwa tayari kutekeleza maombi hayo, wakaendelea kumshikilia. Walijifanya Wamesahau mtu gani wanaeshindana nae.

Carlos akiwa kwake Beirut alipata hasira kudharauliwa na Ufaransa. Akaanzia hapo hapo Beirut, tarehe 15 March mwaka huo akavamia kituo cha utamaduni cha Ufaransa kilichopo Beirut, akalipua jengo zima ambalo mpaka kesho Wafaransa wameshindwa kulinyanyua.
[​IMG]

Week 2 baadae Carlos akapaa kuelekea Paris, Ufaransa akitumia passport ya Uingereza. Siku hiyo raisi mstaafu wa Ufaransa Jacques alikua akisafiri kutoka Paris kuelekea Touluese, na Carlos alipata taarifa kuwa raisi atatumia usafiri wa treni. Target ya kwanza ya Carlos akiwa Paris ni kuteka treni hilo, kisha akalipua kwa bomu, shambulio lililosababisha vifo vya maafisa watano wa serikali na majeruhi zaidi ya 77. Bahati nzuri raisi mstaafu alihairisha safari yake.

Siku hiyo hiyo Carlos na timu yake walilipua gari la gazeti la Al-Watan Al-Arabi na kusababisha kifo cha mtu mmoja na majeruhi 63.

Dec 31 1983 Carlos aliukaribisha mwaka 1984 kwa furaha kubwa, alitekeleza shambulio jingine hatari Ufaransa. Aliteka na kulipua stesheni ya treni na magari ya Marseille Saint-Charles, watu wawili walifariki na 33 kujeruhiwa.
[​IMG]

Siku hiyo hiyo treni itokayo Marseille kuelekea Paris nayo ilitekwa na kulipuliwa, shambulio lililosababisha vifo vya watu watatu na 12 kujeruhiwa. 

Siku hii isingeisha bila kulipua Maison de France iliyopo Berlin, Ujerumani na kusababisha kifo cha mtu mmoja na majeruhi 22.
[​IMG]

Keshowe siku ya sherehe ya mwaka mpya, Carlos alituma ujumbe kwa vituo vitatu vya habari watangaze kua mashambulio yote hayo matatu yeye ndiye anahusika kama ishara ya kulipa kisasi.

Wafaransa bado walishikilia msimamo wake wa kutomwachilia mkewe, ambaye alihukumiwa kifungo cha miaka minne jela. Carlos nae hakuvumilia, akashusha tena shambulio jingine ambapo alilipua duka la bidhaa (shopping mall) Paris.

Carlos aliendelea kuwatesa Ufaransa hadi ilifika kipindi pesa maalumu ikatengwa kwenye bajeti ya Ufaransa kwajili ya kuongeza vifaa na ufanisi ili kumkamata Carlos, vyote hivi havikusaidia. 

Mpaka kufika hatua hii, Carlos alikua adui namba moja wa dunia (most wanted fugitive).

May 4 1985, mke wa Carlos Magdalene Kopp aliachwa huru baada ya kuonesha nidhamu ya kuridhisha, kisha akaungana na Carlos nchini Hungary. 

Kipindi hiki hakikuwa kizuri kwa Carlos, kwani alikuwa amefulia vibaya sana kutokana na kufariki kwa raisi wa Iraq ambaye alikua ni jamaa yake wa karibu, pia hali ya uchumi wa Libya ulikua umedorora sana hivyo Gaddafi hakuweza kumfadhili tena.

Hali ya usalama wake haukuwa mzuri, hivyo aliamua kukimbilia Syria, Aug 17 1986, mkewe akajifungua mwanae wa kwanza. Wakiwa Syria, waziri wa Ulinzi ulimuomba sana Carlos atulie, aache matukio ya ugaidi na ikiwezekana astaafu kabisa, lasivyo Syria isingekuwa tayari kuendelea kumlinda.

Hiki kilikuwa Kipindi kigumu zaidi kwa Carlos, miaka mitano bila kufanya shambulio. Kama wasemavyo waswahili "Jasiri haachi asili".

1990 serikali ya Iraq chini ya Saddam Hussein alimfata Carlos Syria wafanye kazi. Mpango mzima ulikuwa ni Iraq kuishambulia Kuwait. Carlos asingeweza kukataa dili hilo, akalamba dola mil 2 ya Saddam kama advance ya makubaliano ya dola mil 5.

Mipango ya Saddam hussein ilivuja kwenye mashirika ya usalama na ujasusi ya Ulaya ikiwemo DGSE ya Ufaransa. Hali hii ilitishia usalama wa Carlos hadi kumlazimu akimbilie Sudan ambapo aliishi kwenye handaki huko Khartoum.

Kukamatwa kwa Carlos.

Akiwa Sudan taasisi za kijasusi za Ufaransa, DGSE na Marekani, CIA zilitangaza dau kubwa sana kwa utawala wa Sudan kama wangefanikisha kukamatwa kwa Carlos. Sudan hawakuwa na ujanja wa kukataa.
[​IMG]

1994 Carlos alifanyiwa upasuaji mdogo kwajili ya ugonjwa wa tezi dume katika hospitali ya taifaya Sudan. Siku mbili baada ya upasuaji, maafisa wa usalama wa Sudan wakamtaarifu Carlos kwamba anabidi ahamishwe kwenda makazi mapya wakihofia shambulio la kifo lililopangwa kumuuwa, pia waliahidi kumpa ulinzi binafsi.

Carlos hakukataa. Usiku huo mlinzi mmoja ambaye alikuwa afisa wa usalama alimvizia na kumchoma sindano ya usingizi na kukata mawasiliano ya mwili kwa masaa 24. 

Usiku huo serikali ya Sudan ikawasiliana Waziri wa ulinzi wa Ufaransa kwamba Carlos yupo chini ya mikono yao. Alisafirishwa usiku huo huo kuelekea Ufaransa. Keshowe Carlos alipata ufahamu akiwa amezengukwa na maafisa wa usalama wa Ufaransa Paris, mikono na miguu yote imezungushwa pingu.

Hukumu

Dec 1997 Carlos alipatikana na hatia na kushtakiwa kifungo cha maisha bila parole.

Mwaka 2001 Carlos aliamua kumrudia Mungu, na kuwa Muislam. Mwaka huo huo akamuoa mwanasheria wake Isabelle ambae ni wakili nguli sana.[​IMG]

Akiongea kutoka chumba chake cha magereza, Carlos alimtaja Bin Laden kuwa mrithi wake katika vita dhidi ya ubeberu (imperialism) wa mataifa ya magharibi.

Kanali Muamar Gaddafi aliwahi kusikika akisema "Marekani ni nchi yenye nguvu sana, si kama Libya ama Iraq, lakini ukiamua kuwaonesha kuwa unachukizwa na matendo yao, mtoe Carlos jela, mwekee bastola mezani mpe pesa na sigari...kisha washa TV ufuatilie breaking news"

Huyu ndiye mbweha Carlos, Ilyich Sanchez Ramirez mtaalamu wa mapinduzi aliyeitikisa dunia kwa miongo mitatu.
[​IMG]

wafahamu wa ghana alio isumbua idara ya usalama wa marekani kwa miaka 10


Sept mwaka jana ilikuwa mara yangu ya kwanza kukanyaga ardhi ya Marekani. Kuna vitu viwili-vitatu nikuwa navifanya pale Arlington City, Washington DC.
[​IMG]
Nikiwq nakatiza mitaa ya Crystal City, DC.

Nikiwa na mwezi mmoja tu tangu nimalize shahada yangu ya UDSM, sikuwa na familia (mke + watoto), sikuwa na assets kama hati ya nyumba, shamba, kiwanja na kadhalika, hivyo nilipitia vikwazo vingi sana hadi kupatiwa visa ya Marekani. Kitu kimoja kilichonisaidia ni kwamba nilikuwa nimesajili kampuni ya biashara, operations zilikua zimeanza miaka miwili iliyopita, na account ya biashara ilikuwa ina digits zisizo na shaka, biashara ilikuwa tayari ina assets za kutosha za kuprove kuwa lazima nitarudi nchini. Hivyo nikafanikiwa kuwa granted visa ya Marekani daraja B-1/B-2.[​IMG]

Kimsingi ili kupata visa ya US inabidi uthibitishe beyond reasonable doubts kuwa ukisafiri kwenda US utarudi nchini kwako ndani ya muda uliopanga na si kuzamia.

Process nzima ya kupata visa haikuwa lelemama, ulikuwa ni mchakamchaka ambao kiukweli unanyima usingizi.

Tuendelee...

Kwanza kabisa niseme tu wazi, mimi ni 1st generation katika familia/ukoo wetu kwenda US, hivyo sikuwa na guidance yoyote, sikufahamiana na mtu yoyote ambae angeweza kuniongoza, sikuweza kufetch experience yoyote, hivyo ilinilazimu nikomae kivyangu.

Process ya kupata Visa ilianza kwa kujaza online form inayoitwa DS 160 iliyopo kwenye web ya embassy ya Marekani. Ile form ni ndefu sana, ina maswali mengi mno, mengi yalikuwa ni very technical na ya kiintelijensia sana. Niliumiza kichwa sana kuhakikisha naijaza kwa umakini. Nilitumia karibu siku 5 hadi kuisubmit - hata kabla sijaisubmit niliirudia mara 10_10.

Baada ya kusubmit hatua iliyofuata ilikuwa kwenda Citi bank ipo pale Posta, nikalipa $160. Baada ya kulipa nikapata codes fulani ambazo nilizitumia kuomba interview slot. Nakumbuka siku ya interview niliomba iwe Jumatano saa 2 asubuhi.

Hapo tayari nimeshapata tetesi jinsi ambavyo Waafrika wananyimwa visa ya Marekani, nikaGoogle kwamba Marekani wanaingiza $56 mil kila mwaka kutoka Afrika kwa visa vinazokataliwa. Nilikuwa na hofu kubwa sana, hasa nikizingatia nilikua kipindi ambacho sitaki kupoteza hata 'Jero'.

Siku ya interview nikajiandaa vizuri sana, tayari nimekunywa nondo za kutosha kutoka Google, nikabeba makabrasha na documents zangu zote, nikavaa kiheshima haswaa (vijana wa kileo wanasema 'mapigo ya kifaza'), nikafika pale embassy hata kabla ya muda (kuzuga kuonesha kuwa sina mambo ya kiafrika ya kuchelewa).

Pale nilipigwa search ya kufa mtu, nikaacha vitu vyote security nikaingia sehemu ya kusubiri interview. Ni eneo la wazi ambapo watu wote waliopangiwa kufanya interview siku hiyo wanakaa.

Tuliokuwa na interview siku hiyo tulikuwa kama watu 30, kulikuwa na msanii mmoja maarufu (sitamtaja jina), pia alikuwepo mtoto mmoja maarufu wa Raisi Nyerere na pia alikuwepo jamaa mmoja wa TISS ambae yeye alitumwa na waziri fulani (huyu jamaa hakupitia process zozote, aliweka documents zake pale pa'kufanyiwa interview, akapewa maelekezo kisha akasepa).

Kabla interview hazijaanza tuliweka kaplatform uchwara tukawa tunadiscuss mambo kadha wa kadha hasa uchaguzi wa US. Yani mimi ndio nilijiona kilaza, kuna jamaa anajua vitu vyote inside-out vinavyoihusu US na blah blah kibao. Alikuwa anamwaga nondo kuhusu Marekani, miji yake, utamaduni wa Wamarekani, Siasa za marekani, akaanza kutoa 'tips' za maswali ya interview ya kupata visa (nilikuja kugundua kuwa huyu jamaa ni member humu JF - japo sikuweza kung'amua identity yake). Hakika Huyu jamaa alinipa hofu sana, nilihisi kwa nilivyo 'shallow' lazima nitanyimwa Visa - nikajipange vizuri zaidi.

Pia kuna mama mwingine tulikuwa nae akawa anasema alivyojaribu kuomba visa na kunyimwa kila mara, ile ilikuwa mara yake ya 5 anaitwa kwenye interview. (Kumbuka: ukiwa rejected kwenye interview, inabidi urudi uanze application upya na utalazimila kulipa $160 upya), kwa mantiki hiyo, mama yule tayari alitumia $640 kuapply visa). Swala la huyu mama liliniongezea hofu, sikutaka tena story za kijiwe cha mule ndani. Nikajitenga pembeni nikachukua vitabu fulani vya utalii vilikuwa pale nikawa nasoma soma.

Sasa muda wa interview ukaanza, mtu mmoja mmoja anapita kwa ndani kidogo, kuna kidirisha (kama bank kwa teller), then anaanza kuhojiwa na wafanyakazi wa pale embassy. Mtu anayekubaliwa visa basi analazimika kuacha passport yake pale na kupangiwa tarehe ya kuja kuchukua visa yake. Asiyekubaliwa anapewa vitu vyake vyote aondoke navyo.

Katika watu 30, mimi nilikuwa wa 23. Watu wengi walionitangulia walikuwa wananyimwa visa, wengine hadi wanalia pale dirishani. Kiukweli kwenda US ni kama 'dream come true' kwa sisi ambao tulitokea 'the other side of poor neighbourhoods'.

Yule jamaa wa JF aliyekuwa anajua vitu vyote vya States akafika pale dirishani akiwa na mbwembwe nyingi, anapiga kingereza kidogo kisicho na kigugumizi tofauti na mimi. Sikuweza kusikia mahojiano yao, lakini Kitu kilichonistua yule jamaa alirudi na passport yake mkononi, kuashiria kua amenyimwa visa. Pale matumaini ya kupata visa yakaniishia kabisa, moyo ukafadhaika sana. Yule mtoto wa Nyerere aliacha passport yake pale, lakini pia yule msanii alinyimwa.

Zamu yangu ikafika. Moyo ulikuwa unatokota na uwoga 'si wa nchi hii'. Nilivyofika pale dirisha la interview yule jamaa akagundua nina hofu ya hali ya juu sana.

Mahojiano yakaanza. (Hapo ninatetemeka kwa hofu na woga).

Consular: Morning!

Mimi: Yes! Morning

Consular: Akatabasamu kidogo, kisha akauliza - Your sir please!

Mimi: Nikiwa sijitambui nikajibu - Yes sir please .

Jamaa akasmile tena, akaniuliza kwa kiswahili cha kuunga unga. Aiseee!! Hapo nilifunguka si mchezo.

Tulivyoendelea na conversation ndivyo nilivyozidi 'kugain momentum' hadi nikawa kwenye hali yangu ya kawaida.

Statement ya mwisho ikawa "Congratulation sir, you've been granted the US visa, leave your passport with me, and you'll collect it tomorrow together with your visa". Aisee! Feeling ile ilikuwa ya kipekee sana sana. keshowe nilivyokuja kuchukua visa tulikuwa watu wanne tu kati ya wale 30 tuliofanyiwa interview.

Lakini still baada ya kupata visa yangu nilijiuliza sana kwanini US inatubania kupata visa zao?
Kwanini processes ni nyingi mno? kwanini gharama ni kubwa mno?
Je hakuna alternative ya kuingia US bila usumbufu wote huo?

After all sikujali sana kwa sababu tayari nilishapata visa yangu, na vile isingenisaidia kitu kuhoji masharti kila nchi inayojiwekea katika kukaribisha wageni.

Lakini kitu kilichonishangaza zaidi ni wakati nilipofika DIA - Dulles International Airport.

Nikiwa kwenye foleni wakati wa passport control nikamuona black mmoja kasimamishwa muda mrefu sana pale dirishani kwa 'immigration official', lakini white walikua wanapita fasta sana (hata hawakuchukua zaidi ya dakika 1).[​IMG]

Zamu yangu ikafika. Nilipofika tu pale dirishani jamaa kwanza aliniangalia usoni kwa sekunde kadhaa na mimi nikamkazia jicho, 'mubashara' (live) kabisa bila kupepesa kope. Akaniomba passport, nikampa. Akaipitia page baada ya page - kisha akaniuliza "What took you to all these countries?". Kwasababu nilijua nipo 'clean' na nina makaratasi yote muhimu, nikamjibu kwa dharau "I cleared it out when I was in those countries, now I'm in the US - ask me about US". Jamaa akaScan kwanza passport yangu, then akaendelea kunihoji maswali yake ya kiintelijensia. Mimi wala sikutaka kuongea sana, hasa ukizingatia ngeli imekaa kushoto , nilichokifanya ni kumjibu kila swali kwa maelezo machache na kumpa makaratasi. Nilikaa pale kwa dakika 16 - to be exact.[​IMG]

Nilivyoruhusiwa nilijiuliza sana, kwanini hawa jamaa wako 'so arrogant' na nchi yao na wanadharau sana. Nilitamani na sisi waAfrika tuwe na kauwezo ka kuwashikisha adabu na kuwakomoa hawa jamaa.[​IMG] Muonekano wa nje kutoka kwenye dirisha la hotel room nilipofikia

Watoto wa Accra wakanipa sababu ya kuwadharau Marekani na vyombo vya ulinzi na usalama.

Jumanne Nov 8 2016 dunia yote ikielekeza macho kufuatilia uchaguzi mkuu wa Marekani. kuna jambo kubwa sana lilitokea Accra ambalo lilikosa 'Air time' mubashara kutokana na media zote kuelekeza nguvu kwenye uchaguzi mkuu wa uraisi. Tukio hili la kustaajabisha, lililosukwa kwa akili kubwa sana na wahuni wa Ghana, na lilinipa sababu ya kuwaona Wamarekani ni 'watupu'.

Kwa zaidi ya muongo mmoja bendera ya marekani ilikuwa inapeperushwa nje ya jengo kuu-kuu la rangi ya pink katikati ya mji mkuu wa Ghana, Accra.

Mgeni yeyote aliyeingia ndani ya jengo hilo alikutana na picha kubwa ya Rais Barack Obama ikining'inia ukutani. Mapokezi-mezani kulikuwa na kitabu cha wageni chenye seal halali ya idara ya ulinzi ya Marekani. Kila mgeni alikabidhiwa coupon yenye maelekezo, na mwisho kulikuwa na maandishi "Welcome to the US embassy in Ghana".[​IMG]

kijana machachari na mipango ya kibabe

Mwaka 2004 kijana wa umri wa miaka 23 aitwae Yaw Kwabedo anahitimu shahada ya sheria ya chuo kikuu cha Ghana - idara ya sheria. Alihitimu akiwa mmoja wa wanafunzi wenye ufaulu wa juu zaidi darasani kwake.

Kama ilivyo kwa vijana wengi wa Afrika Magharibi, Yaw alikua na ndoto na matamanio ya kwenda na kufanya kazi Marekani kama mshauri wa masuala ya kisheria katika makampuni makubwa.

Aliandaa makabrasha yake yote muhimu, kisha akaanza mchakato wa kupata visa ya Marekani. Aliomba visa mara 4 lakini alinyimwa, alipoteza kiasi kikubwa cha pesa lakini bado aliziishi ndoto zake. Ilimbidi auze baadhi ya mali za nyumbani kwao ikiwemo simu pamoja na runinga, kisha akaomba visa kwa mara ya 5. Lakini bado hakufikia vigezo, akanyimwa tena. Aliumia mno.

Kwabedo aliamini fika kuwa Ubalozi wa Marekani umemdharau na kumdhalilisha. Hivyo, 'piga - uwa - galagaza' atafanya kila awezalo kulipiza kisasi ambacho aliamini lazima angeidhalilisha marekani katika uso wa dunia. Aliapa gharama zake zote alizotumia kuomba visa na kunyimwa zingerudi, pamoja na fidia juu. Aliapa kuwawezesha waghana wote watimize ndoto zao za kuishi Marekani.

Kisasi kinasukwa kwa ustadi wa hali ya juu sana

Feb 2005, Yaw akiwa anatimiza miaka 24 alimwita rafiki yake wa karibu ambaye alihitimu mafunzo ya uhandisi wa kompyuta, kisha akamshirikisha wazo lake ambalo lililenga kuidhalilisha Ubalozi wa Marekani, Idara ya ulinzi na usalama pamoja na vyombo vya kiintelijensia vya Marekani. Huyu rafiki alisita sana akihofia uwezo na nguvu waliyonayo Maafisa wa ulinzi wa Marekani. Lakini Yaw alifanikiwa kumshawishi, na wakaendelea na mipango.

Yaw alihitaji funding, hivyo aliwaingilia watu wenye uhasama na Marekani na kuwashirikisha mpango wake, aliwaendea Waturuki, akawafafanulia vizuri ramani nzima ya mpango aliousuka. Dili likakubali. Hawa Waturuki pia wakaleta jamaa zao Waholanzi wakaunganisha nguvu na resources.

Yaw akaingia Ghana akakodi jengo kubwa lilolopo barabarani kabisa. Akajenga mlingoti kisha akaning'iniza bendera ya Marekani. Material aliyotumia inafikirisha sana - ukiwa mbali ni bendera ya Marekani iliyopungua namba ya nyota _ kati ya zile nyota 50, na kadri unavyozidi kuisogelea rangi inafifia hadi mwisho ukiifikia inakuwa bendera ya Ghana.[​IMG]Jengo lililopeperushwa bendera ya marekani kwa miaka 10.

Yaw akawaomba waturuki wale watafute 1st grade fingerprint scanner. Yule mhandisi akapewa jukumu ya kutambua software systems zinazotumiwa na Ubalozi wa Marekani. Kisha Wakazinunua kutoka kampuni kubwa ya Marekani ya mitandao. Hivyo waliweza kung'amua processes zote zinazotumiwa na wafanyakazi wa Ubalozini (consular).

Nje ya jengo lile Yaw akafunga satellite 2 za usalama, na pia nje kidogo ya lile jengo akafungua duka dogo la kuuza nguo na viatu.

Wakakodi apartment za hali ya juu na kununua magari kadhaa ya kusafirisha abiria.

vyombo vya ulinzi, usalama na uhamiaji vilivyodhalilishwa

Mwaka 2006 mpango mzima unaanza kutekelezwa rasmi. Yaw na team yake wakaanza kuingia mavyuoni, mitaani, vijiweni, vijijini, mjini pamoja na nje ya balozi halisi ya Marekani na kuzungumza na Waghana waliotoswa visa ya kuingia Marekani.[​IMG] Ubaalozi halisi ya Marekani nchini Ghana.

Wote waliokubali mpango wa kina Yaw wakawasafirishwa hadi Accra karibu na ofisi yao, wakawapa hifadhi katika apartment walizokodi pamoja na chakula.

Kisha kila asubuhi walifatwa kutoka wanapoishi na kupelekwa ofisini, huko michakato ya kutengeneza visa bandia ilifanyika kwa ustadi wa juu sana.

Waliweza kufoji vyeti vyote kwa kiwango cha daraja la kwanza, kuanzia taarifa za kibenki, hati za umiliki wa mali, hati za kuzaliwa, vyeti vya daktari, barua za mialiko, barua feki za kupata kazi na admissions za chuo n.k.

Kwa umakini uliotukuka, visa ya kwanza ilitengenezwa, kisha mteja akalipiwa gharama zote za kuingia Marekani na team ya Yaw. Huyu alitolewa kama chambo kuthibitisha uhalisia wa visa hiyo. Baada ya masaa 26 ya safari, Yaw alikenua meno yote 32, pamoja na timu yake wakapiga mvinyo wa pamoja baada ya yule jamaa waliyemtoa chambo kupokelewa na kukaribishwa Marekani kwa visa yao waliyoipika jikoni.[​IMG]Sampuli tu ya visa ya Marekani.

Lengo la muda mrefu la Yaw lilionekana kutimia. Mamia kwa maelfu ya Waghana wakawa wanachongewa visa za kuingia US. Huduma yao ikashamiri hadi nchi za jirani kama Cote d'Voire, Togo na Nigeria. Baada ya muda kidogo nchi za mbali kama Kenya, S.A, India, Palestine, Cameroon n.k. nazo zikaanza kupatiwa huduma.

Wakaanza kujitangaza chinichini kupitia vipeperushi, billboards na magazeti ya udaku. Yaw na timu yake wakaanza kupiga pesa ndefu sana, wateja walimiminika si kawaida. Ilifika kipindi gharama zikapanda hadi kufikia $6000, watu bado walimwagika - walipiga pesa sana. Hakika idara ya Ulinzi (department of Defence) ilidhalilishwa kupita maelezo, tena na kijana wa kawaida kabisa, mbaya zaidi - hawakudhalilishwa kwa masaa kadhaa ama siku kadhaa, bali ndani ya miaka 10 na miezi kadhaa.

Marekani anaamka usingizini - Operation Spartan Vanguard.

Nov 15, 2015 idara ya uhamiaji inashtuka baada ya kugundua kua kuna idadi kubwa sana ya wananchi wa baadhi ya nchi wanapata vibali vya kuingia Marekani, ilhali nchi hizo awali hazikuwa na idadi kubwa ya wananchi wake wanaoingia Marekani.

Upelelezi unaanza... Idara ya ulinzi inatoa tamko la kusitisha kutoa visa kwa baadhi ya nchi kwa muda wa mwezi mmoja. Mshangao mkubwa unaibuka; balozi hazitoi visa, lakini kuna watu bado wanaingia Marekani kwa visa mpya kabisa zinazoonesha wamezitoa ubalozini.

Msako 'wa kufa mtu' unapigwa, wasafiri wote wenye visa mpya kutoka nchi ambazo Marekani ilisitisha kutoa visa zao wanaanza kupelelezwa (interrogated). Pole pole wakaanza kukusanya taarifa, hadi wakafika conclusion kuwa kuna wahuni Ghana ndio wamesababisha fedheha hiyo kwa nchi kubwa yenye ulinzi wa hali ya juu zaidi.

Uvamizi katika ubalozi bandia wa Marekani - Vyombo vya usalama vya Marekani vilitambua fika kua Yaw na timu yake hadi kuweza kufanikisha zoezi la kuidhalilisha Marekani, walijipanga sana. Hivyo, hata wao walibidi 'wajikoki' haswa wasijekudhalilika tena. Zoezi zima la uvamizi halikuwa la 'kispoti spoti'.

Uvamizi huo ulipewa jina la 'Operation Spartan Vanguard'. Kiufupi, operation 'spartans' zote huanzishwa na Marekani kwenye mashambulizi ambayo vikosi vya usalama vimeshindwa kabisa kupata taarifa za awali juu ya eneo wanalopanga kushambulia, hivyo wanajipanga vizuri sana na kwa tahadhari ya juu kwakuwa wameshindwa kumsoma vizuri adui yao. Mara nyingi operatins hizi hazinaga mwisho mzuri. Mfano ni :- Operation Spartan Shield, Operation Spartan Strike, Operation Spartan Fury, Operation Spartan Jordan n.k.[​IMG] Wanajeshi katika 1 ya operation spartan.

Kikosi cha maangamizi kilishiba haswa, hawakufahamu kuwa adui zao ni watu 'walaini'. Kikosi kiliundwa na askari wa Ubalozi wa Marekani, maafisa wa polisi wa Ghana wenye mafunzo ya kijeshi ya Marekani, Taasisi ya upelelezi ya Ghana (Ghana detective bureau), kikosi cha kimataifa maalumu kwa kupamba na uhalifu, askari wa Ubalozi wa Canada, Askari wa uhamiaji wa Marekani pamoja na INTERPOL.

Tena na tena kwa mara nyingine Marekani anadhalilishwa, dunia nzima inamkodolea macho. Kina Yaw wanaisambaratisha Marekani kiulaini kabisa.

Yaw pamoja na timu yake wakiwa ndani ya ofisi yao, tayari walielewa mchezo mzima uliokuwa unaendelea, hawakuwa na papara, hawakuhutaji kujaza risasi kwenye magazine zao. Waliweza kutazama movie nzima wakivamiwa 'mubashara' (live) kupitia satellite mbili walizotegesha nje ya jengo lao.

■ Satellite ya kwanza ilionesha eneo la kuingia ndani ya ofisi yao. Hivyo adui asingeweza kuwafikia bila wao kumshtukia.

■ Satellite ya pili ilionesha usalama la eneo lao la siri la maficho.

Walivyoona wanavamiwa walimuita mmoja wa kijana wa kazi kisha wakampa kichupa, na kumuagiza akifungue kisha akitupe kwenye 'dustbin' ambayo ilikua mlango wa kuingilia. Kichupa hiko kilikuwa ni 'lachrymation spray' - hii ni chemikali kali sana yenye kusababisha muwasho mkali mno sehemu za wazi za mwili (macho, masikio, pua, skin pores, na yale mashimo mengine ya ndani ya c.hupi).[​IMG]askari wa Spartan vanguard wakihenyeshwa.

Baada ya hapo Yaw na team yake wakatoroka kupitia 'built in tunnels' - mifereji ya ndani, ambayo ilipita chini kwa chini na kutokea kwenye lile duka la nguo na viatu nje ya ofisi yao. - Baada ya hapo lazima waingie bar kupongezana .

Kikosi kazi kile cha Wamarekani kiliambulia muwasho 'wa upupu' na kuwakamata baadhi ya wafanyakazi ambao wala hawakuelewa shughuli haramu ziliyokuwa zikiendelea mule ndani.

Upelelezi bado unaendelea, hadi leo kiongozi mkuu wa shambulizi la Spartan vanguard hajaeleza kupatikana kwa wahalifu wakuu na dau nono tayari limetangazwa kwa atakayefanikiwa kukamatwa kina Yaw.

Katika uvamizi huo vitu kadhaa vilipatikana vikiwemo passport 190 (kutoka nchi 10 tofauti), printer 5 za kisasa, HD camera, mihuri bandia 75, laptop 8, smartphones pamoja na documents zinginge nyingi.[​IMG]baadhi ya vitu vilivyopakipatikana
[​IMG]

Kinachowaliza zaidi taasisi za usalama za Marekani

Wizara ya ulinzi, kitengo cha uhamiaji na maafisa wa usalama wa Marekani wameshindwa kabisa kung'amua mafumbo yafuatayo;-

○Wahuni wa Ghana wenye teknolojia ya kawaida kabisa wamewezaje kukamilisha zoezi 'sensitive' kama hilo kwa zaidi ya muongo mzima?!

○Wameshindwa kung'amua ni visa ya daraja gani ilikuwa inatengenezwa na wahuni hao?!

○Wameshindwa kabisa kung'amua utofauti kati ya visa halali na visa bandia.

○Wameshindwa kung'amua idadi kamili ya watu walipewa visa hizo, wangapi walirudi nchini kwao na wangapi bado wanaishi Marekani.

○Wameshindwa kung'amua jinsi gani wataweza kuwatambua na kuwakamata waliokabidhiwa visa bandia na kuingia Marekani.

○Watawezaje kumzuia Yaw na team yake kuendelea kuchapisha visa hizo bandia. Vipi kama wakiunganisha nguvu na maadui wao wakubwa?!

○Wameshindwa kabisa kupata 'identity' kamili ya Yaw na team yake. (Kwa kifupi jina la Yaw ni la kufikirika tu - uchunguzi unaendelea).

○Je ni kivipi wataweza kujisafisha na fedheha hiyo katika dunia paba ya kiintelijensia - watawezaje kuficha udhaifu wao??

My take

Wakati dunia nzima ikiiheshimu na kuisujudia marekani katika swala la ulinzi na usalama, bado naamini kuna vitu vingi vinahitaji kuwa 'fixed'. Nakubali Jeshi lao ni pana sana, lina maaskari wengi na wenye uwezo na fitness nzuri, wamewekeza pesa ndefu, wana miundombinu, vifaa, mbinu na teknolojia za hali ya juu, lakini akitokea mtu mmoja tu mwenye nia thabiti, anaweza 'kuwachambua kama karanga', kuwageuza kama chapati na kiwadhalilisha kwa kadri atakavyo machoni mwa kila mtu, tena mchana kweupeee.

-Meanwhile nafuatilia mubashara uzi wa mkuu The bold jinsi Usama bin Laden alivyowashikisha ukuta Wamarekani.

Baadhi ya taarifa nimepakua kutoka Source mbali mbali za internet zikiwemo:-
BBC News How did fake US embassy operate in Ghana for a decade? - BBC News
US Department of staste Regional Security Office Ghana Shuts Down "Fake Embassy"
BBC focus on Africa BBC World Service - Focus on Africa, 04/12/2016 GMT
The Washington post Mobsters ran a fake U.S. Embassy in Ghana for 10 years, flying the flag and issuing visas for $6,000
Pamoja na source zingine nyingi.

WAJUE WAUZA MADAWA YA KULEVYA WALIO TIKISA DUNIA

Labda ulikuwa miongoni mwa watu waliosikia taarifa ya kukamatwa kwa muuza madawa ya kulevya nchini Mexico, Joaquín Guzmán Loera AKA “El Chapo Guzmán”, na ukajiuliza kuhusu wauzaji madawa ya kulevya ambao waliwahi kutokea katika dunia hii.

Wapo wengi ambao walikuwa wauzaji wa madawa ya kulevya, mabilionea ambao mwisho wao ulikuwa mbaya kama Pablo Escobar. Kama ulikuwa huwajui, hii hapa chini ni orodha ya wauzaji madawa ya kulevya hatari ambao wamewahi kuwepo katika dunia hii mpaka sasa.



[​IMG]

FRANK LUCAS AKA Superfly
Unapowazungumzia wauza madawa ya kulevya ambao wamewahi kuishi katika hii dunia basi hutoweza kuliacha jina la mshikaji huyu, Mmarekani, ‘bitozi’, bilionea ambaye utajiri wake mkubwa ulitokana na uuzaji wa madawa ya kulevya.

Jamaa alivuma sana miaka ya mwishoni mwa mwaka 1960 na mwanzoni mwa mwaka 1970. Jamaa alikuwa na washikaji wengi waliokuwa wakipiga biashara hii haramu. Kila siku, alisafirisha madawa ya kulevya kupitia kwenye majeneza ya watu aliokuwa akiwaua na washikaji zake.

Mwaka 1975, jamaa alivamiwa nyumbani kwake, ndani ya nyumba tu kukakutwa kiasi cha dola laki tano (zaidi ya bilioni moja), kwa kipindi hicho, kilikuwa kiasi kikubwa sana cha fedha. Jamaa alipokamatwa, akafungwa gerezani miaka 75 kwa kesi zaidi ya 100 za madawa ya kulevya.

[​IMG]

CHRISTOPHER COKE AKA: “Dudus”

Jamaa alikuwa mpiga dili mkubwa tu kwenye biashara ya madawa ya kulevya. Alikuwa Mjamaika, mwenye sura ya kipole, kusaidia watu ambapo baada ya kugundulika kwamba anafanya biashara hiyo, hakutaka hata kutafutwa, mwenyewe akajipeleka polisi mwaka 2010.

Mshikaji aliingiza kiasi kikubwa cha fedha, mpaka kukamatwa kwake alikuwa ameingiza kiasi cha dola bilioni 30 (zaidi ya trilioni 60) ambapo kwa sasa tungesema kwamba yeye ni tajiri wa 18 duniani.

Japokuwa alikuwa na ubaya wake wa kufanya biashara hiyo haramu lakini mshikaji alikuwa mtu wa watu. Alikuwa akijenga hospitali, kufanya biashara nyingine na kuwaajiri watu wengi, aliwasaidia masikini na kuwafurahisha kwa kuyaboresha mazingira yao japokuwa upande wa nyuma, aliteketeza vijana kwa kuwauzia biashara hiyo.

[​IMG]

GRISELDA BLANCO AKA: “The Cocaine Godmother”


Unaweza kumchukulia poa tu kwa sababu ni mwanamke lakini ni lazima ujue kwamba kwa watu waliokuwa wakifanya biashara ya kulevya kwa kiasi kikubwa huwezi kumuacha huyu mwanamke.

Alikuwa mtu wa dili, mbali na uuzaji wa madawa hayo, pia alikuwa muuaji mzuri tu ambaye kwa kipindi chote cha kufanya biashara yake, aliwaua watu 200 kwa risasi, tena kwa mkono wake mwenyewe.

Baada ya kufanya biashara hiyo kwa miaka kadhaa, akakamatwa na kufungwa miaka 20 gerezani, ila cha kushangaza sasa, akiwa hukohuko nyuma ya nondo, michongo yake ya biashara ilikuwa ikisonga kama kawa.

Mwaka 2004 akatolewa gerezani lakini ilipofika mwaka 2012, akauawa kwa kupigwa risasi na mshikaji aliyekuwa akiendesha pikipiki. Huo ukawa mwisho wake, akazikwa ingawa bado anajulikana kama mfanyabiashara mkubwa wa biashara hiyo haramu.



Siyo huyu unayemjua wewe! Siyo yule jamaa mwenye mwili mkubwa, mwanamuziki wa Kimarekani, achana na huyo, mshikaji mwenyewe alilichukua jina la Rick Ross kutoka kwa huyu jamaa.

Mwili mdogo, mtanashati, alipenda kutabasamu lakini nyuma ya tabasamu lake, jamaa alikuwa ‘mbaya’ kwenye biashara ya madawa ya kulevya.

Jamaa alianza kufanya biashara hiyo miaka ya 1980. Alianza kama ‘punda’ yaani mbebaji lakini baadaye akajizatiti na kuwa na biashara yake mwenyewe. Jamaa alikuwa akiuza mzigo wa dola milioni 3 (zaidi ya bilioni 6) kila siku iendayo kwa Mungu. Mshikaji alikuwa akiuza kilo 400 kila wiki.

[​IMG]


Arturo Beltrán Leyva AKA: “Boss of Bosses”

Kama washikaji wa hapo juu, hata huyu mwana alikuwa nuksi kwenye uuzaji wa madawa ya kulevya. Mshikaji alikuwa na kundi lake liitwalo Beltran Leyva Cartel, kundi lililosumbua sana nchini Mexico.

Kulikuwa na kesi nyingi dhidi ya kundi hilo, watu walikuwa wakiuawa, wanawake walibakwa, walisafirisha sana silaha kwenda sehemu mbalimbali, wengine waliteswa na kutekwa. Kwa kifupi, kundi hili lilikuwa hatari zaidi kuliko makundi mengine yaliyowahi kutokea huko.

Jamaa aliuawa na wanajeshi wa majini mwaka 2009 katika majibizano ya kurushiana risasi na wanajeshi hao.

[​IMG]

Felix Mitchell AKA: “The Cat”

Jamaa alikuwa si kitoto, huyu ni miongoni mwa wauza madawa ya kulevya wakubwa waliowahi kutokea duniani. Alikuwa na kundi lake liitwalo 69 Mob. Jamaa alikuwa akipiga dili za chinichini, ilikuwa vigumu kukamatwa kwani alikuwa mjanja kupindukia.

Alipokamatwa, alifungwa jela miaka mingi tu ila wakati akiwa ametumikia kifungo kwa miaka miwili, kuna jamaa hukohuko jela akamuua kwa kumchoma kisu, hiyo ilikuwa mwaka 1986 na mazishi yake yalihudhuriwa na watu wengi, sawa na mazishi ya aliyekuwa mwanaharakati, Martin Luther King Jr.

[​IMG]


Amado Carrillo Fuentes AKA: “Lord of the Skies”

Alikuwa Mmexico aliyekuwa akifanya biashara ya madawa ya kulevya kwa kiasi kikubwa. Hakuwa mkuu wa kitengo, aliajiriwa na bosi wake aliyeitwa Rafael Aguilar Guajardo ila akaamua kumuua na kushikilia yeye hicho kitengo.

Ndiye muuzaji pekee wa madawa ya kulevya aliyekuwa akiingiza kiasi kikubwa nchini Marekani kuliko mtu yeyote.

Alikuwa bilionea, mwenye kupenda watu na kusaidia masikini. Hakuwa na utani katika biashara hiyo, aliua wote aliohisi kwamba walikuwa watu wabaya katika biashara yake.

Alitumia ndege zake kusafirisha madawa ya kulevya kwenda nchini Marekani mara nne kwa siku. Kumkamata haikuwa kazi nyepesi kwa sababu alikuwa akibadilisha sura yake kwa kuvaa sura ya bandia.

Mwaka 1997 alipokuwa akifanyiwa upasuaji wa kuwekewa sura ya bandia katika Hospitali ya Santa Monica nchini Mexico, dawa zilizidi hivyo kufariki dunia na baada ya siku mbili, wale madaktari waliofanya upasuaji huo wa kumuwekea sura ya bandia wakakutwa wameuawa kinyama na miili yao kutupwa.

[​IMG]

Pablo Escobar AKA: “The World’s Greatest Outlaw”
Huyu jamaa alikuwa kiboko, ni Mcolombia aliyekuwa akiuza madawa ya kulevya kwa kiasi kikubwa. Alikuwa katili, kuua watu waliokuwa kinyume naye ilikuwa ishu ndogo sana kwake.

Hakutaka mchezo, hakuwahi kuweka fedha benki, alikuwa akizihifadhi ndani na wakati mwingine zilikuwa zikiliwa na panya. Kuna kipindi mtoto wake alikuwa akiumwa, alizitumia dola za Kimarekani kumuwashia moto, eti kupoza baridi lililokuwa likimpiga, kitu kilichowakasirisha sana Wamarekani, waliona wamedharauliwa sana mpaka noti yao kuchomwa moto.

Alikuwa na utajiri mkubwa na mwaka 1989 alitangazwa kama tajiri wa saba duniani akiwa na utajiri wa dola bilioni 25 (zaidi ya shilingi trilioni 50). Jamaa alikuwa akimiliki 4/5 ya soko kubwa la madawa ya kulevya duniani.

Jamaa alikuwa akisafirisha tani 15 za madawa ya kulevya kila siku barani America. Jamaa aliua majaji 30 waliokuwa wakisimamia kesi zake na polisi 400 ambao walionekana kimbelembele kumfuatilia kwenye mishe zake na pia aliilipua ndege aina ya Avianca Flight 203 ambayo ilikuwa ikimbeba waziri mkuu wa kipindi hicho nchini Colombia.

Kwa kifupi, jamaa alikuwa na pesa ndefu kiasi cha kuiambia serikali yake kwamba imuache afanye mishe zake kwani angelipia deni la dola bilioni 20 (zaidi trilioni 40) lililokuwa ikidaiwa, ila serikali ikakaata na kumuua.

[​IMG]

Joaquín Guzmán Loera AKA “El Chapo Guzmán”


Hapa ndipo kwenye kazi sasa. Huyu anaonekana kama mwamba wa biashara hii ya madawa ya kulevya. Ni Mmexico mwenye mkwanja mrefu ambapo amekuwa akiupata kupitia biashara yake haramu.

Alikuwa mtu anayetafutwa kwa nguvu zote kabla ya kukamatwa. Aliwekeza nguvu kubwa katika biashara hii, Wamarekani na Wamexico walimtafuta lakini hawakumpata.

Wakati wakiwa na uchungu naye, wakafanikiwa kumpata na hivyo kufungwa nchini Mexico. Kutokana na fedha alizokuwa nazo, inasemekana kwamba aliwahonga askari magereza na kutoroka kwa kupitia katika bomba la choo, unaamini hilo?

Wamarekani walikasirika sana, wakaahidi kumtafuta, kweli wakaingia mzigoni. Hawakuchukua muda sana, wakamnasa na hivyo kuiambia Serikali ya Mexico kwamba watamfunga wao wenyewe ili wamuonyeshee kwamba wao si watu wa mchezo, kweli wakamfunga na mpaka leo hii yupo gerezani akiendelea kutumikia kifungo chake ambacho hakikuwekwa wazi ni cha

jionee picha za zamani[TBT] za paul makonda



mbunge atoa pendekezo condom zipigwe marufuku tanzania

[​IMG]
Mwakilishi Nadir Abdul-latif Yussuf Alwardy, CCM wa Jimbo la Chaani aliitaka Serikali ya Zanzibar kupiga marufuku Condoms, uuzwaji na usambazaji ikiwa kweli jamii inataka kulidhibiti tatizo la ubakaji na udhalilishaji wa jinsia kwa vijana na watoto.
Amesea kuzagaa kwa Condom mitaani ni kichocheo kikubwa kinachowamasisha vijana kufanya vitendo vya kudhalilishana ovyo ovyo wakijua kuwa wao watabaki salama.

Alisistiza kuwa matumizi ya Condom yatumike kwa kibali maalum cha Daktari tu.

Rais Magufuli ashiriki ibada ya Jumatano ya majivu Mt Petro

[​IMG]

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisali katika Ibada ya Jumatano ya Majivu pamoja na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Benjamini Wiliam Mkapa, Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa na Mke wake Mama Janeth Magufuli katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Petro lililopo Oysterbay jijini Dar es Salaam.

[​IMG]
[​IMG]

[​IMG]

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Benjamini Wiliam Mkapa wakiwatakia heri ya Masista katika Ibada ya Jumatano ya Majivu iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Parokiya ya Mtakatifu Petro lililopo Oysterbay jijini Dar es Salaam.

[​IMG]

[​IMG]

[​IMG]

[​IMG]

[​IMG]

Paroko Msaidizi wa Kanisa la Mtakatifu Petro Father Asis akijiandaa Kumpaka majivu kichwani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika Ibada ya Jumatano ya Majivu iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Parokiya ya Mtakatifu Petro lililopo Oysterbay jijini Dar es Salaam.
[​IMG]

Paroko Msaidizi wa Kanisa la Mtakatifu Petro Father Asis akimpaka majivu kichwani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika Ibada ya Jumatano ya Majivu iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Parokiya ya Mtakatifu Petro lililopo Oysterbay jijini Dar es Salaam.

[​IMG]

Paroko Msaidizi wa Kanisa la Mtakatifu Petro Father Asis akimpaka majivu kichwani Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli katika Ibada hiyo ya Jumatano ya majivu.

[​IMG]


Paroko Msaidizi wa Kanisa la Mtakatifu Petro Father Asis akimpaka majivu kichwani Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Benjamini Wiliam Mkapa katika Ibada hiyo ya Jumatano ya majivu.

[​IMG]

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Benjamini Wiliam Mkapa mara baada ya Ibada hiyo ya jumatano ya Majivu iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Ads Inside Post