Jumatano, 1 Machi 2017

yanga na simba zilivyogonganisha viongozi wa siasa na serikali












Hivi ndivyo timu za yanga na simba zilivyowakutanisha baadhi ya viongozi wa serikali pamoja na viongozi wa chama cha upizani cha chadema









kweli steve nyerere anaishi kisaniii


Steve Mengere ‘Steve Nyerere’

WATU wengi walipigwa na butwaa na kubaki midomo wazi baada ya kuvuja kwa sauti inayodaiwa kuwa ni ya mchekeshaji Steve Mengere ‘Steve Nyerere’ na mama mzazi wa muigizaji Wema Sepetu.
Audio ilikuwa ya kawaida tu, lakini kilichofanya ionekane ishu, ni kule kuwahusisha watu wazito kwenye nchi hii na sakata la kukamatwa na baadaye kushtakiwa kwa matumizi ya bangi, kwa Wema. Kama ilivyotarajiwa, Steve Nyerere alitumia uungwana, akatoka mbele ya jamii na kuomba radhi.
Wasanii wa Bongo muvi katika kampeni ya Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu ‘Mama ongea na mwanao project’
Hicho ndicho kitu pekee ambacho alipaswa kukifanya, vinginevyo angekuwa mtu wa ajabu ‘kukausha’ ili kuacha upepo upite kama pepo zingine zinavyopita. Na niseme ukweli, utetezi wake pia nimeupenda, maana amesema kweli kuwa ilibidi atumie sanaa ili kumuweka vizuri mama ambaye aliishi naye vizuri kama mwanaye.
Ni vile tu mama Wema aliwahi kusema, lakini hata mimi nilikuwa najiuliza kwa kutomuona Steve akienda kumsabahi dada yake pale Central au hata kumsindikiza mahakamani. Historia inanionyesha huyu mchekeshaji huwa hakosi katika matukio yanayomhusisha Wema Sepetu na mara kadhaa, ameonekana akiwa karibu na mama Wema. Yes, ilibidi atumie sanaa ili kumuweka sawa na alifanikiwa.
Steve Nyerere wa kwanza (Kulia) katika mradi mwingine na wasanii/watu maarufu
Kwa hiyo, alichojaribu kusema ni kuwa yote aliyoongea ndani ya sauti ile, ni uongo. Kwamba hakwenda Dodoma, hakuongea na mawaziri waliotajwa wala wabunge na kwamba kilichotokea hakihusiani kwa namna yoyote na yeye. Lakini katika uhalisia wake, kuna uhusiano mkubwa wa kilichosikika na kilichotokea, ingawa siyo hoja ya leo hapa.
Ninachotaka tuwekane sawa, ni namna gani Steve Nyerere anapata mkate wake wa kila siku. Ukimsikiliza wakati akizungumza na waandishi wa habari, alisema yeye anaishi kwa sababu ya jina lake, alilotumia miaka mingi kulitengeneza. Steve ni muigizaji wa filamu na mchekeshaji. Huku kwenye filamu hajawahi kuwa staa wa kuuza sana kiasi cha kusema anaishi maisha tunayomuona kwa sababu hiyo.
Lakini pia kwenye uchekeshaji, siku hizi kuna kitu kinaitwa Stand Up Comedy, ile ambayo msanii anawajaza watu ukumbini na yeye kuanza kuwachekesha. Wanafanya hivi pia waigizaji wengine ambao kwa Afrika Mashariki, kinara wao ni Eric Omondi wa Kenya, Anna Kasiime wa Uganda na hapa nyumbani, MC Pilipili pia hufanya. Siku hizi Steve Nyerere naye anafanya Stand Up Comedy.
Steve Nyerere
Ni kwa kiasi gani Stand Up Comedy ya Steve inamuingizia hela ni jambo la kujadili. Steve anaishi sababu ya jina lake kwa kufanya kazi za sanaa au anaishi kisanii? Kuna uwezekano mkubwa pia kwamba licha ya sanaa, Steve anaishi kisanii, ndiyo maana sanaa aliyosema aliitumia katika kumuweka sawa mama Wema, inafanana sana na maisha yake halisi.
Steve anafika sehemu ambazo wengi hawawezi kufika na anazungumza na watu ambao siyo kila msanii anaweza kuwafikia. Watu wote waliotajwa katika ile sauti wanaweza kufikiwa na huyu msanii bila matatizo yoyote, ingawa zipo pia chumvi za kutosha katika hilo.
Unashangaa kumuona Steve Nyerere akipanda katika jukwaa la muziki na kuanza kumtunza mwimbaji manoti mengi mithili ya wale mapedeshee tuliowazoea, kina Chief Kiumbe, Papaa Msofe, Muzamir Katunzi, Jack Pemba, Ndama Mutoto ya Ng’ombe na wengine wa aina hiyo.
Kutoa ni moyo na si utajiri, lakini ni kweli kijana wa Kitanzania anayepata hela kwa jasho lake kihalali, anaweza kugawa fedha nyingi kwenye starehe kama Steve anavyofanya? Ingawa siungi mkono hata kidogo kitendo kilichofanywa na Mama Wema, ni vyema nikamtahadharisha Steve kwamba kilichotokea halikuwa jambo la bahati mbaya. Yale ndiyo maisha yake, ya kutumia sanaa yake.
Na huenda siyo kwa mama Wema pekee, sanaa hiyo yaweza kuwa imetumika ‘kuwaweka’ sawa pia watu kibao ambao hatuwafahamu!

Tunda amlipua steve nyerere

  1. Wakati sakata la audio inayosemekana ni mazungumzo baina ya mtu anayesadikiwa kuwa steve nyerere na mama wa wema sepetu kuvuja, Video queen maarufu nchini, Anna Patrick maarufu kama Tunda amemjia juu steve nyerere na kumtolea maneno ya shombo baada ya steve kusikika kwenye audio iliyovuja akimponda tunda kuwa ni mjinga kukubali kurubuniwa na makonda na kupewa mil 2.,amemchana kupitia mtandao wa instagram[​IMG]
     

wasanii bongo movie wamkana wema sepetu


  1. Wasanii wa filamu za Kibongo, leo wameitisha mkutano na waandishi wa habari ambapo wamekanusha kuidai CCM huku wakisema kwamba wote walilipwa.
    Tazama video...

    Wasanii Bongo Movies Wampinga Wema Sepetu, Wakanusha Kuidai CCM

    MOVIE BADO INAENDELEA: Hivyo ndivyo tunaweza kusema baada ya wasanii wa Bongo Movie Wasanii wa Bongo Movies waliokuwa wakishiriki kwenye kampeni ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 ya Mama Ongea na Mwanao ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kukanusha taarifa iliyotolewa na Wema Sepetu kuwa CCM haijawalipwa pesa za kampeni walizofanya kwenye uchaguzi huo.

    Wakizungumza na waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Protea, wasanii hao wakiongozwa na Yobnesh Yusuph ‘Batuli’ na Ndumbangwe Misayo ‘Thea’, wamesema madai aliyoyatoa Wema Sepetu hayana ukweli wowote kwa sababu wasanii wote walilipwa na Wema alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa wakiwalipa wasanii hao.

    Mara baada ya Thea na Yobnesh kuzungumza maneno machache, mkutano huo na waandishi wa habari ulimalizika, ukiwa umechukua dakika chache tu na kuacha kila mtu akaizungumza lake.

    “Ni kweli inasemekana kwenye mitandao kuwa tulifanya kampeni na hatukulipwa, mimi kama Mwenyekiti Msaidizi wa Muda, nakanusha taarifa hizo kuwa si za kweli… wapo wanaoshawishiwa kulichafua kundi letu, kumchafua Makamu wa Rais Bi. Samia Suluhu na kuichafua CCM, mimi nakataa, sote tumelipwa na mikataba ipo.

    “Zipo simu za kushwishiwa kuhama lakini hatutohama chama na Kundi la Mama Ongea na Mwanao litaendelea kuwepo chini ya Usimamizi wa Bi. Samia Suluhu.” Alisema Batuli.

    Wema Sepetu alivyohamia Chadema.

    Hivi karibuni msanii wa Bongo Movie, Wema Sepetu aliibuka mbele ya wanahabari wakati akihamia Chadema kwa madai ya kufanyiwa hila kwenye CCM huku akidai kuwa Kundi la Mama Ongea na Mwanao linakidai CCM pesa yao ya kampeni waliyofanya mwaka 2015.

    Steve Nyerereakikanusha taarifa za kukidai CCM.

    Aidha siku moja baadaye msanii wa filamu na mchekeshaji maarufu Bongo, Steve Nyerere aliyekuwa mwenyekiti wa Kundi hilo wakati wa kampeni aliibuka na kukanusha taarifa za wasanii wa Bongo Movie kukidai CCM huku akieleza kuwa wasanii wote walilipwa pesa zao kama mikataba iliyokuwa ikieleza.

nyumba ya mama wema yapigwa mawe kwa saa nzima



  1. MAMA mzazi wa mrembo wa Tanzania mwaka 2006 Wema Sepetu, Mariam Sepetu, usiku wa kuamkia jana nyumba yake iliyopo maeneo ya Sinza Mori jijini Dar es salaam imepigwa mawe juu ya bati kwa muda wa saa moja na nusu.

    Akizungumza na MTANZANIA nyumbani kwake jana alisema kuwa usiku wote huo alikosa raha na kupata hofu kubwa na kuhisi kuna watu wabaya ambao walikuwa wanataka kumvamia na kujikuta akikosa usingizi.

    “Nimekosa usingizi na hofu juu huku simu yangu iliishiwa salio kwani nilikuwa nikitaka kupigia simu ndugu na majirani ili waje kunisaidia, sikuweza kutoka nje kwa kuwa sikuwa najua mbaya wangu amekaa wapi na amekusudia kufanya nini,” alisema.

    Baada ya kupambazuka alitoa taarifa kwa mwanae Wema na viongozi wengine wa Chadema ambapo Meya wa Ubungo, Boniface Jacob alifika ili kuangalia hali ya mama huyo na kuamua kumuwekea ulinzi.

    “Tumeshaangalia mazingira yote tumegudua kitu ambacho hatuta kiweka wazi kwa sasa ila tutaweka ulinzi mkali na atakaye jaribu shauri yake hatuta kubali suala hili liendelee kumkuta kamanda wetu na mimi mara kwa mara nitafika kuangalia mazingira,” alisema Jacob.

    Meya alifafanua zaidi kuwa ulinzi huo hautaishia nyumbani kwa mama Wema, bali hata nyumbani kwa Wema ulinzi utaimarishwa, kwa sababu wamegundua wanachama hao wapya wamekuwa wakiwindwa na watu wasiojulikana.

    Kwa upande wake Wema alipohojiwa alisema, anashindwa kuelewa hao watu waliofanya kitendo hicho walikuwa wanataka nini kutoka kwao.

    “Mama yangu ameteseka usiku kucha kwa kukosa amani, amelia na kukosa hata hamu ya kula tumefika tumemkuta katika hali mbaya, najua yana mwisho ila tutazidi kufanya dua ya kumwomba Mungu atuepushe na mabaya yote,” alisema Wema.

hii ni maalum kwa wanaume wanaopenda six pack

  1. Majukumu na lifestyles zetu hua zinaweza kupelekea fat ikajikusanya mno tumboni na kupelekea kutokea kitambi au tumbo ambalo tunakua hatujaridhika nalo.
    Ikifika hatua hiyo tunachotakiwa ni kuiondoa hiyo fat hapo ilipo ili kupata lile tumbo ambalo litaridhisha macho yetu.

    Haya mazoezi yanaweza kufanywa kokote na jinsi zote wanaweza wakafanya.

    Jua kwamba.
    Kuna mazoezi mengi ya kupunguza tumbo, haya ni yale ambayo nayatumia mimi hivyo mengine yapo modified kwa kadri mimi ninavyoyafanya.

    Kisayansi six packs hazihesabiwi kama ni alama ya mtu kua ni mwenye afya, hii ni kwa kua unakua umeondoa fat yote tumboni ambayo tumbo lako huihitaji. But fvck science on this one.

    Na-assume sisi ni beginners, kama uko advanced ongeza idadi ya reps (30).

    Kanuni Yetu Ni Hii.
    -Kila zoezi litakua na seti tatu.
    -Kila seti moja itakua na reps 10 mpaka 12.
    -Kupumzika kati ya reps na reps ni sekunde 15.
    -Kupumzika kati ya zoezi na zoezi ni dakika moja.

    Tuanzeni...

    Kuendesha Tairi.
    9k%3D.jpg
    Utakua ukianza kwa kurudisha nyuma tairi na kukipeleka mbele kiasi mgongo wako unakua umenyooka. Ukipeleka mbele ukikirudisha hiyo ni moja.
    Kwa sisi ambao hatuna balansi, napendekeza upande tunaojinyoosha kuwe na kitu cha kutuzuia ili tusiende chini moja kwa moja mfano kukiwa na ukuta itakua vizuri zaidi.
    Hapa tunafanya reps 10 kwa seti tatu.

    Crunches.
    Unakua umelala chini magoti yameinuka, unaunyanyua mwili nusu, yaani sehemu ya kiuno inakua hauiinui.
    Sit_up_Crunch_M_WorkoutLabs.png
    Unakua unainuka lakini bila lengo la kuyafikia magoti yako. Ukinyanyuka na kurudi chini hiyo ni moja.
    Hapa tunafanya reps 12 mara tatu.

    Crunches Miguu Juu.
    Unakua umelala ila miguu inakua juu ya kitu, sehemu miguu itakayokaa isikufanye kuuinua mwili wako iwe adhabu mimi huwa naweka juu ya kitanda.
    Ukiwa gym unaweza chagua benchi la kuwekea miguu yako.
    200px-Crunches-2.png
    Kama utaweza kuinuka mpaka kuifuata miguu yako na kuishika itakua vizuri, kama hauwezi panda kiasi cha kiuno chako kisiwe kimelala chini. Kama bado hauwezi fanya kama ulivyotoka kufanya zoezi lililopita.
    Hapa tunafanya reps 10 mara tatu.

    Sit ups.
    Unakua umelala na miguu umeinyanyua, hapa utanyanyua mwili wako wote wakati unayafuata magot yako lakini wakati unarudi chini mwili usiguse chini, sehemu ya kiuno na mgongo kidogo ndiyo utakua unailaza sakafuni.
    img_20150410_163518.jpg
    Hapa kurelax hupatikana kutokana na ukali wa mbinuko wa magoti tuliouweka, mfano mbinuko wa kwenye hiyo picha kwa anayeanza ni mkali mno.
    Tunafanya reps 10 mara tatu.

    Sit Ups Nusu Nusu.
    Hizi nilizimodify kutokana na mahitaji yangu, hilo jina nimetunga hapa hapa (sorry).
    Inakua sawa na zoezi lililopita isipokuwa hapa tunanyanyua mwili na kuishia kati kisha tunarudi chini baada ya hapo tunaanzia pale kati tulipokua tunaishia na kuyafuata magoti.
    IMG_20170201_091400.jpg
    (Samahani sijui kuchora.)
    Hapa tunafanya za kutokea chini na kuishia kati reps 6 na kuanzia hapo kati kueleka magoti reps 6. Tutafanya hivyo mara tatu.

    Sit Ups Tatu kwa Moja.
    Hii ni nyingine ambayo niliimodify.
    Utalala chini kama kawaida ila Miguu yako utaitanua kiasi cha kuweza kuona mbele.
    1485932262367.jpg
    Utakua ukinyanyuka mikono yote unapeleka upande wa kushoto, unarudi chini.
    Ukinyanyuka tena mikono unapeleka upande wa kulia, unarudi chini.
    Ukinyanyuka mikono utapitisha kati kati ya miguu.
    Hiyo ni moja.
    Tutafanya hivi reps 3 mara tatu.

    Oblique Sit Ups.
    oblique-situp1.jpg
    Tunafanya kama zoezi lililopita, ila hapa utakua ukiinuka kuyafuat magoti yako kiwiko cha mkono wa kulia kitakua kinaenda upande wa goti la kushoto na kiwiko cha upande wa kushoto kitakua kinaenda upande wa goti la kulia.
    Mfano, Utakua unanyanyuka kiwiko cha kulia kitaenda upande wa kushoto, utarudi chini, utanyanyuka tena kiwiko cha kushoto kitaenda upande wa kulia, utarudi chini. Hiyo ni moja.
    Tutafanya reps 7 kwa seti tatu.

    NB.
    -Jiandae kwa Maumivu ya tumbo na kuharisha kwa siku moja au mbili.
    -Kama una kitambi kikubwa sana napendekeza main dish ya zoezi lako iwe ni kukimbia mpaka baada ya muda, pia anza na zoezi la 1, 2, na 3 mengine utayaongeza polepole kadri utakavyokua unaendelea.
    -Mapendekezo yangu ya reps na seti unaweza ukapunguza au ukaongeza kulingana na mahitaji yako na uzoefu wako.
    -Natumia uzoefu na kujifunza kwa wengine, sijasomea, ushauri wangu siyo wa kidaktari.

kiama kwa wanywa viroba nchini



Kiama cha washukia wanywaji kilevi cha pombe maarufu kama viroba,onyo hilo limetolewa rasmi na serikali ya awamu ya tano kuwa ni marufuku kuuza ama kununua bidhaa ya kiroba na kama mtu atakamatwa kwa kujihusisha na uuzaji ama ununaji wa kilevi hicho adhabu yake ni faini ya shillingi  500000= elfu hamsini pamoja na kifungo kisichopungua miezi mitatu jela





Ads Inside Post