Alhamisi, 15 Desemba 2016

ifahamu kensa

*Dr. Brian Berry wa Marekani amegundua kensa mpya kwa binadamu inayosababishwa na Silver Nitro Oxide. Unaponunua kadi ya simu usiichune kwa kucha kwani imo hiyo Silver Nitro Oxide na inaweza kusababisha kensa ya ngozi. Watumie ujumbe huu wale uwapendao.*

*Nukuu muhimu za afya*
*��sikiliza simu kwa sikio la kushoto.*
*��usimeze dawa na maji baridi*
*��usile chakula kizito baada ya saa kumi na moja jioni.*
*��kunywa maji mengi asubuhi na kidogo usiku.*
*��wakati mzuri wa kulala ni kuanzia saa nne hadi kumi usiku.*
*��usilale mara baada ya kula dawa au chakula.*
*��ikiwa charge imebakia kijino cha mwisho usipokee* *simu kwani mionzi inakuwa na nguvu kwa mara 1000 zaidi.*
*��unaweza kuwatumia haya wale unaowajali?*
*Mie nimeshafanya.*
*Huruma haigharimu kitu lakini elimu ni nuru.*
*������ MUHIMU ������*
*Jumuiya ya uchunguzi ya marekani imetoa majibu mapya. Usinywe chai kwenye vikombe vya plastic. Na usile Chochote kwenye mifuko ya plastic. Plastic ikikutana na joto inatoa vitu vinavyo sababisha aina 52 za kensa.

uke kutka harufu mbaya

UKE KUTOA HARUFU MBAYA

  

Leo ningependa tuzungumzie tatizo la uke kutoa harufu mbaya, kwani ni tatizo ambalo linawaathiri dada zetu sana, na huwafanya wasiwe na uhuru wanapokuwa faragha na wapenzi wao, na kuwafanya wasiwe na raha, na kupoteza kujiamini.
Tatizo la kutoa harufu ukeni husababishwa na sababu kadhaa Kama ifuatavyo.

1.Bacterial vaginosis
Kwa kawaida, uke huwa na bakteria ambao huitwa lactobacilli, bakteria hawa ni wazuri na hawamletei shida yeyote mwanamke, bakteria hawa huulinda uke usishambuliwe na bakteria wabaya ambao ndio husababisha magonjwa. Kinachowawezesha bakteria hawa waweze kukaa kwenye uke ni hali ya utindikali wa uke(vaginal acidity); hali hii ya utindikali wa uke inapobadilika na kupungua kwa sababu yeyote ile, husababisha bakteria hawa kupungua, na hivyo kutoa nafasi kwa bakteria wabaya kukua kwa wingi, na kushambulia afya ya uke, hivyo kusababisha harufu(harufu hii hutokana na uchafu unaotengenezwa na bakteria hawa).Hali hii kitaalamu ndio huitwa bacterial vaginosis.Ni muhimu kufahamu kuwa ugonjwa huu hauambukizwi kwa njia ya zinaa, japokuwa wanawake ambao wanajihusisha katika ngono wanakuwa katika hatari kubwa zaidi ya kpata ugonjwa huu, pia wanwake wanaofanya “douching”(kujisafisha ukeni kwa kuingiza kidole) na wanaoshiriki mapenzi kinyume cha maumbile wako kwenye uwezekano mkubwa wa kupata bacterial vaginosis.

2.Magonjwa ya zinaa (Sexually transmitted diseases;Vaginal Trichomoniasis, gonorrhea,chlamydia)
Ugonjwa wa zinaa unaoitwa kitaalamu vaginal trichomoniasis ndio ugonjwa wa zinaa ambao unaathiri wanawake wengi zaidi kuliko ugonjwa mwingine wowote wa zinaa. Ugonjwa huu unasababishwa na protozoa anaejulikana kwa jina la Trichomona vaginalis. Na huambukizwa kwa njia ya ngono. Dalili za ugonjwa huu kwa wanawake ni kutoa majimaji yanayotoa harufu kali, yenye rangi ya njano–kijani,kuwashwa ukeni.
Gonorrrhea kwa kawaida pia huweza kusababisha kutokwa na majimaji yenye harufu ukeni, na kuwashwa, maumivu wakati wa kukojoa, maumivu wakati wa kufanya mapenzi, na maumivu chini ya kitovu (japokuwa, kwa gonorhea wanawake wengi wanaweza wasionyeshe dalili yoyote kwa muda mrefu).
Mara nyingi, inaweza kuwa vigumu kwa daktari kuweza kutofautisha baina ya magonjwa haya ya zinaa (hasa kwa mazingira yetu duni); Hivyo basi mara nyingi daktari atatoa dawa kwa ajili ya magonjwa haya matatu ya zinaa pale anapofikiri kuwa mgonjwa wake ana tatizo la ugonjwa wa zinaa.

3.Fangasi za ukeni (Vagina candidiasis)
Fangasi za ukeni pia huweza kusababisha kutokwa na harufu kali ukeni, japokuwa si kwa kiwango kikubwa sana kama sababu mbili hapo juu. Pia, mara nyingi mwanamke mwenye tatizo la fangasi za ukeni atalalamika kuhusu kuwashwa zaidi kuliko harufu.
Dalili za fangasi za ukeni ni pamoja na kutoa majimaji mazito ya rangi nyeupe (kama maziwa mtindi) yenye harufu, kuwashwa ukeni,pamoja na kusikia maumivu wakati wa kufanya mapenzi.
Vitu ambavyo vinamuweka mwanamke katika hatari ya kupata fangasi za ukeni ni pamoja na kufanya “douching” (kujisafisha uke kwa kuingiza kidole), kuvaa nguo za kubana, kuvaa nguo za ndani ambazo sio za cotton, kuvaa nguo za ndani ambazo hazijapigwa na jua/kupigwa pasi, usafi hafifu wa sehemu za siri, matumizi ya vyoo vya kukaa na matumizi ya dawa za uzazi wa mpango.

Je, nini cha kufanya ili kujiepusha na harufu mbaya ya sehemu za siri kwa mdada?
-Epuka kusafisha uke kwa kuingiza kidole ukeni-Uke usafishwe kwa maji ya vuguvugu na sabuni ya kawaida ya kuogea (sio medicated soap), bila kuingiza kidole au kitu chochote ndani ya uke
-Epuka matumizi ya madawa ya antibiotics kwa muda mrefu bila ya kuambiwa na daktari-kwani dawa hizi zikitumika kwa muda mrefu na bila ushauri wa daktari husababisha mabadiliko katika bakteria wa kwenye uke na kupelekea magonjwa na harufu mbaya
-Vaa nguo za ndani za cotton
-Epuka nguo za kubana sana mwili
-Nguo ya ndani ianikwe nje; sehemu ambayo itapigwa na jua (na sio ndani ya chumba); au nguo za ndani zipigwe pasi kabla ya kuvaliwa,
-Unapokuwa kwenye siku zako zingatia usafi na kubadilisha pedi kama inavyotakiwa(mara 2-3 kwa siku)
-Epuka kutumia vyoo vya umma ambavyo ni vya kukaa,
-Jikinge na magonjwa ya zinaa,
-Epuka kuvaa nguo nyingi na/au nzito wakati wa kulala; vaa nguo nyepesi ambayo itaruhusu uke kupata hewa ya kutosha.
-Jisafishe vizuri kila baada ya kumaliza haja ndogo,
-Kitu kingine ambacho ni muhimu sana kufahamu, ikitokea ukaona kuwa uke wako unatoa harufu, kuuosha kwa maji mengi na sabuni nyingi mara nyingi, sio suluhisho bali unazidi kuleta matatizo zaidi kwa sababu unazidi kupunguza idadi ya bakteria wazuri, na kubadilisha hali ya utindikali wa uke na hivyo kukaribisha bakteria wabaya kwa wingi zaidi!!
-Na kitu cha mwisho ambacho ni muhimu zaidi, ni kwetu wanaume, unapoona mwenzi wako ana tatizo hili, usimseme vibaya au kumkaripia au kumtukana; Unatakiwa kutambua kuwa huo ni ugonjwa na umsaidie kuweza kuonana na wataalamu wa tiba kwa

Ads Inside Post